Pata taarifa kuu

Vita vya Israel na Hamas: UNSC kukutana Jumatatu hii usiku

Urusi imesambaza kwa nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa rasimu ya azimio ambalo litapigiwa kura. Rasimu hiyo inatoa wito wa "kusitishwa kwa mapigano mara moja, kudumu na kuheshimiwa kikamilifu" na "bila kuzuiliwa" ufikiaji wa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa, kulingana na shirika la habari la AFP.

Moja ya vikao vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Moja ya vikao vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. ©REUTERS/Shannon Stapleton
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na haki inayoendelea katika Mashariki ya Kati hasa mashambulizi ya jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaz, baada ya kundi la Hamas kushambulia Israel siku kumi zilizopita, Urusi inasema inatiwa wasiwasi na hali hiyo, ambayo inaweza kuwa hatari duniani.

Hayo yanajiri wakati zaidi ya 1,000 bado hawajulikani walipo chini ya nyumba na majengo yaliyoharibiwa katika mashambulizi ya anga ya Israel.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani inayoendeshwa na Hamas huko Gaza, pia alithibitisha kwamba idadi hii ya watu haikupatikana.

Takriban Wapalestina 2,750 wameuawa na 9,700 wamejeruhiwa tangu Oktoba 7 huko Gaza, wizara ya afya ya Palestina imesema leo, na kuongeza kuwa 58 waliuawa na zaidi ya 1,250 wamejeruhiwa katika Ukingo wa Magharibi.

Miongoni mwao, 11 walikuwa waandishi wa habari wa Kipalestina, kulingana na Chama cha Waandishi wa Habari wa Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.