Pata taarifa kuu

Putin kufanya mazungumzo na viongozi wa Israel, Iran, Misri, Syria na Mamlaka ya Palestina

Rais wa Urusi Vladimir Putin anatarajiwa leo Jumatatu, Oktoba 16 kuzungumza, kwa njia ya simu na rais wa Misri Al-Sissi, kiongozi wa wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, baada ya kuwaita wakati wa mchana viongozi wa Iran Ebrahim Raïssi na Bashar  Al-Assad wa Syria.

Rais wa Urusi Vladimir Putinanasema anafuatilia kwa karibu hali ya Masharuiki ya Kati hususan huko Gaza.
Rais wa Urusi Vladimir Putinanasema anafuatilia kwa karibu hali ya Masharuiki ya Kati hususan huko Gaza. AFP - MIKHAIL METZEL
Matangazo ya kibiashara

"Rais (wa Urusi) tayari amezungumza na marais wa Syria na Iran," amesema mshauri wa kidiplomasia wa Kremlin Yuri Ushakov, aliyenukuliwa na mashirika ya habari ya Urusi. "Wakati wa mchana, bado kutakuwa na mzungumzo ya simu na (...) Al-Sissi na (...) Abbas, pamoja na Waziri Mkuu wa Israel," ameongeza, limesema shirika la habari la AFP.

Hayo yanajiri Umoja wa Mataifa umesema mzozo kati ya Israel na Hamas umefikia hatua mbaya wakati hospitali za Gaza zikikaribia kuishiwa akiba ya nishati na juhudi za kupitisha misaada ya kiutu katika mpaka wa Rafah zikiendelea.

Madaktari kwenye Ukanda wa Gaza wametahadharisha kwamba huenda maelfu ya watu wakapoteza maisha ikiwa hospitali zilizojaa watu waliojeruhiwa zitaishiwa mafuta na mahitaji mengine muhimu.

Umoja wa Mataifa kupitia Katibu Mkuu Antonio Guterres umetoa wito kwa kundi la Hamas liwaachilie huru mateka huku ukiitaka Israel kuruhusu misaada ifike katika Ukanda wa Gaza. Guterres amesema Umoja huo una chakula, maji, dawa na mafuta ambayo tayari yako Misri na katika ukingo wa magharibi kwa ajili ya kupelekwa Gaza kama wafanyakazi wake wataruhusiwa kuvisafirisha bila ya vikwazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.