Pata taarifa kuu
MAZUNGUMZO-AMANI

Beijing inasema inataka kushirikiana na Misri katika Mashariki ya Kati

China ilifanya mazungumzo na Misri wiki hii na inataka kufanya kazi nchi hii kutafuta suluhu la vita kati ya Israel na Hamas, mjumbe wake wa Mashariki ya Kati amesema, akitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano.

Kikosi cha wanajeshi wa Israeli katika wakipiga kambi huko Kfar Aza, Oktoba 10, 2023.
Kikosi cha wanajeshi wa Israeli katika wakipiga kambi huko Kfar Aza, Oktoba 10, 2023. © Thomas Coëx / AFP
Matangazo ya kibiashara

Zhai Jun alizungumza kwa njia ya simu Jumanne na Osama Khedr, mkurugenzi wa idara ya masuala ya Palestina katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri ambaye aliteuliwa kuwa balozi wa Israel mwezi Agosti, kulingana na ripoti ya mazungumzo iliyotolewa na mamlaka ya China.

China iko tayari kudumisha mawasiliano na uratibu na upande wa Misri ili kuhimiza usitishaji mapigano kati ya pande hizo mbili zinazohusika na mzozo huo haraka iwezekanavyo," amesema Zhai Jun. Pia ametoa wito kwa "jumuiya ya kimataifa kuwek mapoja juhudi za kutoa msaada wa kibinadamu kwa Wapalestina, ili kuepusha kuzorota zaidi kwa mzozo wa kibinadamu huko Palestina, hasa katika Ukanda wa Gaza.

Idadi ya vifo kutokana na vita kati ya Israel na Hamas imeendelea kuongezeka kwa kasi siku ya Jumatano, huku maelfu ya vifo vikirekodiwa kwa jumla, siku nne baada ya shambulio lililoanzishwa na vuguvugu la Kiislamu la Palestina kutoka Gaza.

Idadi ya vifo kutokana na mashambulizi nchini Israel imeongezeka na kufikia zaidi ya "watu 1,200," jeshi la Israel limetangaza siku ya Jumatano asubuhi. Kwa upande wa Wapalestina, watu 900 wameuawa na zaidi ya 4,500 wamejeruhiwa, kulingana na mamlaka za ndani.

Tangu shambulio hilo, Misri imeongeza juhudi zake za kidiplomasia kujaribu kuzima ghasia hizo. Kwa muda mrefu Misri imekuwa mpatanishi wa jadi kati ya Israel na Hamas, na ilikuwa nchi ya kwanza ya Kiarabu kutia saini makubaliano ya amani na Israel mwaka 1979. Pamoja na Israel, imedumisha kizuizi cha Ukanda wa Gaza tangu mwaka 2007.

Kwa upande wake, diplomasia ya China, ambayo mapema mwaka huu iliwezesha maelewano ya kustaajabisha kati ya Iran na Saudi Arabia, mara kwa mara inasema inataka kutoa mchango wake katika mchakato wa amani kati ya Israel na Palestina, ambao umesimama tangu mwaka 2014.

Hadi hivi karibuni China ambayo ilihusika kidogo katika suala la Israel na Palestina ikilinganishwa na Marekani, inadumisha uhusiano mzuri na Israel, na sasa inasisitiza msimamo wake kuhusu suala hilo kwa nguvu zaidi.

Wakati wa wito wake siku ya Jumanne, Zhai Jun alisema kuwa "msingi wa mzozo wa mara kwa mara kati ya Israel na Palestina ni kuchelewa kupata suluhu la haki kwa swali la Palestina, na matokeo ya kimsingi yanatokana na kutekelezwa kwa suluhisho la serikali mbili."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.