Pata taarifa kuu

Rais wa Iran aalikwa kuzuru Saudi Arabia na Mfalme Salman

Mfalme Salman wa Saudi Arabia amemwalika Rais wa Iran Ebrahim Raissi kufanya ziara rasmi nchini mwake, hatua nyingine katika maelewano ya wazi kati ya madola hayo mawili hasimu ya kikanda.

Rais wa Iran Ebrahim Raisi mjini Tehran tarehe 29 Aprili 2017.
Rais wa Iran Ebrahim Raisi mjini Tehran tarehe 29 Aprili 2017. Atta Kenare/AFP
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Tehran, Siavosh Ghazi

Mwaliko huu umetolewa chini ya siku kumi baada ya uamuzi wa Iran na Saudi Arabia kurejesha uhusiano wao wa kidiplomasia. Hakuna tarehe iliyobainishwa kwa wakati huu. Lakini mambo yanaonekana kwenda haraka tangu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir Abdollahian, atangaze kwamba atakutana na mwenzake wa Saudia hivi karibuni.

Mnamo Machi 10, nchi hizo mbili zilitangaza kurejesha uhusiano wao wa kidiplomasia ndani ya miezi miwili baada ya mazungumzo ya siri huko Beijing. Tangu wakati huo, kauli chanya zimeongezeka. Wakati huo huo Waziri wa Uchumi wa Saudi ametangaza kwamba Saudi Arabia inaweza kufanya uwekezaji mkubwa nchini Iran.

Mahusiano ya kisiasa na kiuchumi

Baada ya zaidi ya miaka kumi ya kuvunjika kwa uhusiano kati ya nchi hizi mbili, nchi hizozimeamua kufungua ukurasa mpya. Riyadh na Tehran zilipingana huko Syria, Yemen, Iraq, lakini pia nchini Lebanon. Hatua hii ya mabadiliko katika mahusiano ya mataifa hayo mawili yenye nguvu zaidi katika ukanda huo itakuwa na matokeo katika nchi hizi.

Tayari Iran na Bahrain, mshirika wa Saudi Arabia, wameamua kurejesha uhusiano wao wa kidiplomasia. Rais wa Syria Bashar al-Assad akiungwa mkono na Tehran anapokelewa katika Umoja wa Falme za Kiarabu. Iran na Iraq zinapaswa saini makubaliano ya usalama. Ni dhahiri kuwa, nchi za ukanda huo zimeamua kuweka kando tofauti zao ili kuimarisha uhusiano wao wa kisiasa, lakini pia wa kiuchumi, na hivyo kuzitia tumbo joto Marekani na Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.