Pata taarifa kuu
USALAMA-DIPLOMASIA

Ibrahim al-Nabulsi, mbabe wa kivita wa Fatah, auawa katika shambulio la Israeli

Adui namba moja wa Waisraeli ameuawa kwa kupigwa risasi huko Nablus Jumanne asubuhi. Ibrahim al-Nabulsi, mbabe wa kivita wa Fatah, alikuwa amekimbilia katika nyumba moja katika mji unaokaliwa wa Ukingo wa Magharibi. Alifanikiwa kupenya dhidi ya kikosi maalum cha Israel mara kadhaa. 

Nablus, inayokaliwa kwa mabavu Ukingo wa Magharibi: Wapiganaji kadhaa wa Kipalestina kutoka tawi la wapiganaji la Fatah wameuawa katika uvamizi wa jeshi la Israeli, akiwemo mmoja wa viongozi wake, Ibrahim al-Nabulsi, kiongozi mkuu katika Brigedi ya Mashahidi wa Al-Aqsa, Agosti 9, 2022. .
Nablus, inayokaliwa kwa mabavu Ukingo wa Magharibi: Wapiganaji kadhaa wa Kipalestina kutoka tawi la wapiganaji la Fatah wameuawa katika uvamizi wa jeshi la Israeli, akiwemo mmoja wa viongozi wake, Ibrahim al-Nabulsi, kiongozi mkuu katika Brigedi ya Mashahidi wa Al-Aqsa, Agosti 9, 2022. . REUTERS - RANEEN SAWAFTA
Matangazo ya kibiashara

Kwa zaidi ya saa tatu vikosi maalum vya Israel vimezingira nyumba moja huko Nablus kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi. Ndani ya nyumba hiyo alikuwepo Ibrahim al-Nabulsi, afisa mkuu wa Brigedi za Mashahidi wa Al-Aqsa, tawi la wapiganaji wa Fatah na wapiganaji wengine wa kundi hili. Wanajeshi wa Israel waliwataka wajisalimishe, lakini walikataa. Al-Nabulsi alituma ujumbe wa sauti: Nitakufa kama shahidi, msiweki chini silaha, alitangaza.

Majibizano ya risasi yaliripotiwa. Hatimaye roketi ilirushwa kwenye jengo hilo na kumuua kamanda huyo wa Palestina papo hapo. Kulingana na Wizara ya Afya ya Palestina, wapiganaji wengine wawili wameuawa wakati wa shambulio hili na wengine karibu 40 wamejeruhiwa.

Ibrahim al-Nabulsi alikuwa mtu anayetafutwa zaidi na idara za usalama za Israel katika Ukingo wa Magharibi. Alishukiwa kushiriki katika mfululizo wa mashambulizi dhidi ya Israel. Mara kadhaa alikuwa ameponea chupuchupu kukamatwa na jeshi la Israel. Miezi sita iliyopita alinusurika katika shambulio lililolengwa na vikosi maalum vya Israel katikati mwa mji wa Nablus. Saa chache baadaye, alishiriki katika mazishi ya wenzake akiwakejeli wanajeshi wa Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.