Pata taarifa kuu

Mfumuko wa bei mwezi Desemba wasababisha hali kuwa ngumu Uturuki

Kulingana na takwimu rasmi zilizotolewa Jumatatu Januari 3, kupanda kwa bei za bidhaa za chakula kumefikia 36.08% katika kipindi cha mwaka mmoja mwezi Desemba, jambo ambalo halijawahi kutokea tangu mwaka 2002, hasa kutokana na kuanguka kwa sarafu ya pauni.

Wafanyabiashara katika eneo la Eminönü, Istanbul, Uturuki.
Wafanyabiashara katika eneo la Eminönü, Istanbul, Uturuki. AFP - OZAN KOSE
Matangazo ya kibiashara

Mamilioni ya Waturuki wanatatizika kupata riziki, pamoja na chakula, kwani bei ya vyakula imepanda kwa 44%.

Recep Özkan anafuga ng'ombe wa maziwa katika kijiji kilicho kilomita 50 kutoka katikati mwa mji wa Istanbul. Mfumuko wa bei, kwake, kwanza kabisa ni ongezeko la gharama zake za uzalishaji: mbolea, mafuta, malisho ya ndama wake wachanga. Bei za bidhaa hizi zote - nyingi zinazoagizwa kutoka nje - zinapanda siku baada ya siku. Kwa hivyo Recep inabidi afanye maamuzi: “Sikununua mbolea yoyote mwezi uliopita kwa sababu bei imepanda mara tatu. Na ilinibidi kuongeza bei ya maziwa yangu. Inaumiza moyo wangu kwa sababu ninauza moja kwa moja kwa mnunuzi na najua sote tunatatizika kupata riziki. "

Mnamo mwezi Desemba, ongezeko la bei za wazalishaji lilikaribia 80% kwa mwaka mmoja. Ikiwa hali itazidi kuwa mbaya, Recep hana uhakika kama ataendelea kufuga ng'ombe: "Tunakaa karibu na meza, tunafanya hesabu. Pesa tulizotumia, pesa tulizopata. Hatujawahi kupata hasara kama hiyo. Tunapovuna tulichopanda, ikiwa hatuwezi kufidia gharama zetu, najiuluzi ikiwa tunaweza kuachana na kazi hii. "

Na siku zijazo inaonekana kuwa ngumu, hasa kwa kuongezeka kwa gharama za nishati. Mnamo Januari 1, kwa mfano, bei ya umeme nchini Uturuki iliongezeka kutoka 50% hadi 130%.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.