Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Afghanistan: Milipuko mibaya yatokea karibu na uwanja wa ndege wa Kabul

Milipuko miwili imetokea Alhamisi, Agosti 26 katika shambulio "tata" karibu na uwanja wa ndege wa Kabul, makao makuu ya jeshi la Marekani, Pentagon, imesema. Tukio hilo linasemekana kuwa limesababisha vifo vya watu sita, wakiwemo Wamarekani na watoto, na zaidi ya kumi na tano wamejeruhiwa, ameripoti mwandishi wetu huko Kabul, ambaye alikuwa mita 200 kutoka eneo la mlipuko.

Wafanyakazi wa idara ya uokoaji wanawaondoa watu waliojeruhiwa katika milipuko miwili uliolenga uwanja wa ndege wa Kabul Agosti 26, 2021.
Wafanyakazi wa idara ya uokoaji wanawaondoa watu waliojeruhiwa katika milipuko miwili uliolenga uwanja wa ndege wa Kabul Agosti 26, 2021. AFP - WAKIL KOHSAR
Matangazo ya kibiashara

Pentagon na vyanzo vingine vinathibitisha kuwa hii ilikuwa shambulio "tata". Kulingana na vyanzo kadhaa, shambulio lilikuwa shambulio kujitoa muhanga, ambalo limeua watu wasiopungua sita, wakiwemo Wamarekani na watoto, na pia "zaidi ya kumi na tano waliojeruhiwa na watoto kuuawa, ameripoti mwandishi wetu huko Kabul, Vincent Souriau. Mlipuko mwingine ulitokea baadaye, ”ameongeza. Kulingana na Pentagon, "angalau mlipuko mwingine mmoja ulitokea karibu na Hoteli ya Baron, ambayo iko karibu na Lango la Abbey."

Mlipuko umetokea katika lango la kuingilia la abbey ambako vikosi vya Uingereza vimekuwa katika eneo hilo siku za karibuni.

Ni moja kati ya milango mitatu iliyokuwa imefungwa baada ya kuwepo tahadhari ya tishio la kigaidi.

Afisa wa Marekani ameliambia Shirika la habari la Reuters kuwa mlipuko huo ulisababishwa na mtu aliyejitoa muhanga.

Mataifa ya magharibi yalikuwa tayari yameonya juu ya uwezekano wa shambulio katika uwanja wa ndege wa Kabul katikati mwa juhudi za uhamishaji mkubwa wa watu. Nchi kadhaa ziliwatolea mwito raia wake kuepuka maeneo ya uwanja wa ndege, ambako maafisa walidai kulikuwa na kitisho cha bomu la kujitoa muhanga.

Tahadhari hiyo iliyotolewa siku ya Jumatano inalihusisha kundi la Afghanistan lenye mafungamano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS ambalo kuna uwezekano kuimarika kwake kumetokana na kuachiwa kwa wafungwa wengi wa Taliban na uvamizi wao kote nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.