Pata taarifa kuu
UTURUKI-UNESCO-JAMII

Uturuki: Jumba la makumbusho la Hagia Sophia kugeuzwa kuwa Msikiti

Mahakama ya juu zaidi nchini Uturuki imefungua njia ya jumba la zamani la Hagia Sophia kugeuzwa kuwa msikiti na kubadilisha hadhi yake ya sasa kama jumba la makumbusho.

Watu wakiwa wamejifunika bendera za Uturuki mbele ya Jumba la makumbusho la Hagia Sophia, baada ya Mahakama kuchukuwa uamuzi unaofungua njia ya jimba hilo kugeuzwa kuwa Msikiti, huko Istanbul, Julai 10, 2020.
Watu wakiwa wamejifunika bendera za Uturuki mbele ya Jumba la makumbusho la Hagia Sophia, baada ya Mahakama kuchukuwa uamuzi unaofungua njia ya jimba hilo kugeuzwa kuwa Msikiti, huko Istanbul, Julai 10, 2020. REUTERS/Murad Sezer
Matangazo ya kibiashara

Baraza la kitaifa la Uturuki lilikubali ombi la mashirika kadhaa yakiliomba kufuta uamuzi wa serikali wa tangu mwaka 1934 unaolipa jumba la Hagia Sophia huko Istanbul hadhi ya jumba la makumbusho.

"Mahakama imeamua kufutilia mbali uamuzi wa baraza la mawaziri ambao uliogeuza jumba hilo takatifu kuwa jumba la makumbusho," mahakama imesema katika taarifa yake.

Mahakama imebaini kwamba katika vitendo vya mali iliyoandikwa kwa jina la Mehmet Fatih Foundation, iliyopewa jina la mfalme (sultani) wa Ottoman ambaye alitawala eneo la Constantinople katika karne ya 15, jumba la Hagia Sophia liliorodheshwa kama msikiti na kwamba sifa hii haiwezi kubadilishwa.

Kazi kubwa ya usanifu iliyojengwa katika karne ya 6 na watu wa Byzantines waliowapa mataji wafalme wao, jumba la Hagia Sophia ni miongoni mwa maeneo yaliyowekwa kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO, na ni moja wapo ya vivutio vikuu vya watalii huko Istanbul.

Jumba hili ambalo liligeuzwa kuwa msikiti baada ya kutekwa kwa eneo la Constantinople na wapiganaji wa utawala wa Ottoman mnamo mwaka wa 1933, lilibadilishwa kuwa jumba la makumbusho mnamo mwaka 1934 na kiongozi wa Jamhuri changa ya Uturuki, Mustafa Kemal.

Nchi kadhaa, hasa Urusi na Ugiriki, ambazo zinafuatilia kwa karibu hatima ya urithi wa Byzantine nchini Uturuki, na Maarekani na Ufaransa, ziliionya Ankara dhidi ya kugeuza jumba la makumbusho la Hagia Sophia kuwa mahali pa ibada kwa Waislamu, hatua ambayo rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekuwa akitolea wito kufanyika kwa miaka mingi.

Hayo ynajiri wakati Hivi karibuni msemaji wa rais nchini Uturuki Ibrahım Kalın alisema kuwa kufunguliwa kwa Hagia Sophia kama eneo la ibada hakutaipunguzia kwa kiasi chochote urithi wake katika historia ya ulimwengu.

Hayo Kalın aliyazungumza katika mahojiano na kituo cha habari cha Anadolu nchini Uturuki kuhusu mjadala wa eneo hilo lenye historia kubwa duniani kufunguliwa kama msikiti, akisisitiza kuwa kufunguliwa kwa eneo hilo kwa ibada hakutapunguza chochote bali watu wengi zaidi wataweza kuzuru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.