Pata taarifa kuu
UTURUKI-SAUDIA-KHASHOGGI-HAKI

Mahakama ya Uturuki yachunguza mauaji ya Jamal Khashoggi

Mahakama ya Uturuki imeanza kusikiliza kesi ya mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi ambaye aliuawa mwaka 2018 huko Istanbul katika majengo ya ubalozi wa Saudi Arabia nchini Uturuki.

Mwandishi wa habari Jamal Khashoggi alitoweka baada ya kuingia katika ubalozi wa Saudi Arabia huko Istanbul Oktoba 2, 2018.
Mwandishi wa habari Jamal Khashoggi alitoweka baada ya kuingia katika ubalozi wa Saudi Arabia huko Istanbul Oktoba 2, 2018. REUTERS/Osman Orsal/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Kesi hiyo inasikilizwa wakati washtumiwa katika mauaji hayo wako nchini Saudi Arabia.

Maafisa saba wa Saudi Arabia, ikiwa ni pamoja na naibu mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi, Ahmed al Assiri, na mshauri wa zamani wa Mfalme wa Saudi Arabia, al Kahtani, wanatuhumiwa 'kupanga na kukusudia kutekeleza' mauaji hayo.

Washtakiwa wengine 18 wanatuhumiwa kutekeleza mauaji hayo kwa kumkandamiza chini mwandishi huyo anayejulikana kwa ukosoaji wake dhidi ya Mwanamfalme Mohammed bin Salman.

Baada ya taarifa zilizotofautiana, viongozi wa Saudi arabia walikubali kwamba Jamal Khashoggi, ambaye alikuwa uhamishoni Marekani, aliuawa na viungo vyake vya mwili kukatwa katwa Oktoba 2, 2018 na maafisa wa Saudi arabia ambao walitekeleza ukatili huo kwa hiari yao, kulingana na taarifa hizo.

Tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa ilitangaza mwezi Juni 2019 kuwa ina ushahidi tosha kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman alihusika kwa mauaji hayo, huku shirika la ujasusi la Marekani la CIA na nchi kadhaa za Magharibi wakisema kuwa mwanamfalme huyo ndiye aliagiza Jamal Khashoggi auawe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.