Pata taarifa kuu
UTURUKI-MAREKANI-SAUDI ARABIA-JAMAL-HAKI

Erdogan: Mauaji ya Jamal Khashoggi yalipangwa kwa muda mrefu

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema Jumanne (Oktoba 23) kwamba kuna vithibitisho tosha vinavyoonyesha kwamba mauaji ya mwandishi wa habari na mkosoaji mkubwa wa utawala wa Saudi Oktoba 2 ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul, ulipangwa kwa muda mrefu.

Mmoja aw waandamanaji akishikilia picha ya mwandishi wa habari wa Saudi Arabia  Jamal Khashoggi, aliyeuawa Oktoba 2, 2018 katika ubalozi mdogo wa Saudia, Istanbul.
Mmoja aw waandamanaji akishikilia picha ya mwandishi wa habari wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi, aliyeuawa Oktoba 2, 2018 katika ubalozi mdogo wa Saudia, Istanbul. REUTERS/Osman Orsal
Matangazo ya kibiashara

Akifafanua ,mbele ya Bunge matokeo ya uchunguzi kuhusu kifo cha Jamal Khashoggi, Rais Erdogan ameitaka Saudi Arabia kutoa majibu kuhusu ulipo mwili wa Khashoggi na ni nani aliyeamuru oparesheni hiyo.

Rais Erdogan amethibitisha kuwa watu 18 wamekamatwa nchini Saudi Arabia kutokana na kesi hiyo japo hajatoa maelezo zaidi kuhusiana na ushahidi uliotolewa.

Rais Erdogan pia amebaini kwamba kundi la watu 15 wanaosadikiwa kuwa raia wa Saudi Arabia waliwasili mjini stanbul kwa kutumia ndege tofauti siku kadhaa kabla ya mauaji ya mwandishi huyo.

Erdogan amesema mwili wa marehemu inadhaniwa kuwa ulitupwa katika msitu wa Belgrad, karibu na ubalozi wa Saudi Arabia, mjini Istanbul.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.