Pata taarifa kuu
SYRIA-IS-USALAMA

Jeshi la syria lajaribu kuingia Deir Ezzor

Jeshi la Syria limefaulu Jumanne hii kuvunja ngome kuu ya wapiganaji wa kundi la Islamic State yaliyowekwa miaka mitatu iliyopita katika eneo la serikali ya Deir Ezzor, mashariki mwa nchi hiyo.

Askari wa Syria katika mji wa Deir Ezzor tarehe 12 Novemba 2016, wakati wa mapiganona kundi la IS  karibu na eneo la Houwayqa.
Askari wa Syria katika mji wa Deir Ezzor tarehe 12 Novemba 2016, wakati wa mapiganona kundi la IS karibu na eneo la Houwayqa. Ayham al-Mohammad / AFP
Matangazo ya kibiashara

Vladimir Putin "amekaribisha" operesheni ya wakuu wa majeshi ya Urusi na Syria, pamoja na Rais Bashar al-Assad kupitia telegram, kwa "ushindi huu muhimu". Ndege za kivita za Urusi zimetoa msaada mkubwa kwa askari wa Syria.

Ushindi huu ni mkubwa kwa jeshi la Syria na ni kupoteza kwa kundi la Islamic State. Hata kama ngome hii iliyowekwa na wapiganaji wa kundi la IS kwenye eneo hili la kilomita mia moja za mraba imevunjwa, vita bado vinaendelea.

Operesheni iliyoendeshwa na kufaulu siku ya Jumanne itaruhusu kusafirisha chakula na dawa bila kusahau askari wa ziada katika sehemu hii ya mji, wenye wakazi wanaokadiriwa kati ya 150,000 na 200,000. Watu hawa, ambao wanakabiliwa na uhaba wa chakula, madawa na mafuta, wamekua wakihudumiwa kwa njia ya anga kwa miaka mitatu sasa.

Kilomita chache zaidi upande wa kusini, sehemu nyingine ya serikali, ambayo inajumuisha uwanja wa ndege wa kijeshi na wilaya tatu, yenye kilomita mraba 40, bado imezingirwa kabisa. Safu ya jeshi la Syria na washirika wake wanaelekea kusini mwa nchi ili kuvunja ngome hiyo. .

Hatimaye, Deir Ezzor ina hifadhi muhimu zaidi za mafuta nchini Syria. Hii ni chanzo muhimu cha mapato kwa serikali ya Syria, ambayo inahitaji sana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.