Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA

UN yatoa wito kusimamishwa kwa muda mapigano Syria

Umoja wa Mataifa unataka mapigano kusitishwa kwa muda katika mji wa Raqqa nchini Syria ili kupisha misaada na kuruhusu idadi ya raia waliopo katika eneo hilo la mapigano kuondoka.

Marekani na Muungano wa vikosi vya Syria, Kiarabu na Kikurdi wanajaribu kuukomboa mji wa Raqqa kutoka mikononi mwa wapiganaji wa Islamic State.
Marekani na Muungano wa vikosi vya Syria, Kiarabu na Kikurdi wanajaribu kuukomboa mji wa Raqqa kutoka mikononi mwa wapiganaji wa Islamic State. REUTERS/Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

Raia wapatao 25,000 wamekwama ndani ya mji huo wakati ambapo bado kunashuhudiwa mfululizo wa mashambulizi ya anga tangu wiki moja iliyopita.

Shirika la kimataifa la Amnesty linasema mamia ya watu wameuawa tangu mashambulizi hayo yalipoanza katika mji wa Raqqa mwezi Juni mwaka huu.

Mkuu wa misaada ya kibinadamu nchini Syria, Jan Egeland, anasema mji wa Raqqa yawezekana kwa sasa ni moja kati ya maeneo hatari duniani na ametaka hatua za haraka kuchukuliwa ili kutoa nafasi kwa raia kuondoka katika eneo hilo hatari.

Bw. Egeland amesema kuwa wapiganaji wa Islamic State wanatumia kundi la raia waliobaki kama kinga ya kivita.

Wapiganaji wa IS wanatumia raia kama kinga yao katika mapigano hayo, “ amesema Jan Egeland.

Baadhi ya nchi zimeshikamana kwa minajili ya kuukomboa mji huo kutoka mikononi mwa wapiganaji wa Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.