Pata taarifa kuu
SYRIA-LEBANON-USALAMA

Mapigano makali kati ya IS na vikosi vya Lebanon

Jeshi la Lebanon, toka siku ya Jumatatu Agosti 7, linaendelea kushambulia kwa mabomu ngome za kundi la Islamic State kwenye mpaka na Syria. Wapiganaji wa kundi hili wamekua wakijibu kwa kurusha roketi nyingi ardhi ya Lebanon.

Roketi zilianguka katika mji wa Lebanon wa Al-Qaa,katika milima ya Bekaa kwenye mpaka na Syria.
Roketi zilianguka katika mji wa Lebanon wa Al-Qaa,katika milima ya Bekaa kwenye mpaka na Syria. Kate Geraghty/The Sydney Morning Herald/Fairfax Media via Getty
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Lebanon linatumia silaha kubwa za kivita dhidi ya ngome zinazoshikiliwa na wapiganaji wa kundi la Islamic State katika milim aya vijiji vitatu kwenye mpaka na Syria. Wapiganaji wa kundi la Islamic State wamekua wakijibu kwa kurusha roketi nyngi katika mji wa al-Qaa, unaokaliwa na watu wengi kutoka jamii ya Wakristo. Roketi nne zimeanguka ndani ya eneo hilo, lakini hazikusababisha hasara yoyote.

Mapigano hayo yanakuja wakati ambapo suaa muhimu lililopo ni operesheni kabambe ya jeshi la Lem=banon kwa minajili ya kuwatimua wapiganaji wa kundi la Islamic State kutoka eneo la milima lenye kilomita mraba 400, ambapo, nusu ya eneo hilo iko nchini Lebanon.

Kulingana na vyanzo vya usalama kutoka Lebanon, karibu maelfu ya wapiganaji wa kundi la Islamic State wamekimbilia katika msitu ulio kati ya Lebanon na Syria. Wiki iliyopita, jeshi la Lebanon lilianza kurusha mabomu dhidi ya ngome za kundi la Islamic State, kwa msaada wa ndege za kivita.

Jumanne hii, Rais waLebanon Michel Aoun anatazamiwa kukutana na mamlaka ya juu ya usalama nchini, ambayo ni Baraza kuu la Ulinzi, ambalo linaweza kuruhusu kuanzisha mashambulizi kabambe dhidi ya kundi la Islamic State.

Hali hii inatokea ndani ya wiki mbili baada ya mashambulizi ya kundi la Hezbollah katika ukanda huu dhidi ya kundi la zamani la Al-Nosra Front. Mapigano hayo yalimalizika kwa kuwahamisha mamia ya wapiganaji wa kundi hilo na familia zao, sawa na watu 10,000 kwa jumla, kwenda mkoa wa Syria wa Idleb.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.