Siha Njema
Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi nchini Kenya wakati wa janga la Corona
Imechapishwa:
Cheza - 10:04
Baraza linaloongoza mapambano dhidi ya Ukimwi nchini Kenya ,National Aids Control Control Council, limesema Kenya imeripoti mambukizi mapya zaidi ya elfu 41 mwaka wa 2021, hii ikikuja wakati wanaharakati wa kupambana na Ukimwi wakihofia mvutano kati ya serikali na wafadhili, ambao umesababisha uhaba wa dawa za ARVS na kondomu unatishia pakubwa mapambano hayo.