Pata taarifa kuu
SRI LANKA

Mkutano wa nchi za Jumuiya ya Madola waanza mjini Colombo licha ya baadhi ya nchi kuususia

Hatimaye mkutano wa nchi wanchama za Jumuiya ya Madola umefunguliwa rasmi hii leo mjini Colombo nchini Sri Lanka licha ya hapo awali nchi kadhaa kutangaza kususia mkutano huo kutokana na rekodi mbaya ya nchi hiyo kwenye haki za binadamu. 

Rais wa Sri Lanka, Mahinda Rajapaksa
Rais wa Sri Lanka, Mahinda Rajapaksa EUTERS/Dinuka Liyanawatte
Matangazo ya kibiashara

Mtoto wa mfalme, Prince Charles ndiye aliyefungua mkutano huu akimwakilisha mama yake malkia Elizabeth wa pili ambaye hakuweza kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa mwaka huu ambao ulikuwa umegubikwa na suala la rekodi mbaya ya haki za binadamu kwa nchi ya Sri Lanka.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron tayari amewasili nchini Sri Lanka tayari kwa mkutano huu ambao ajenda kubwa mbali na kujadili uhusiano baina ya nchi wanachama suala la kuheshimu haki za binadamu pia linatarajiwa kujadiliwa.

Kabla ya kuanza kwa mkutano huu, rais wa Sri Linka, Mahinda Rajapaksa alitangaza wazi kuwa nchi yake haitamvulia mtu yeyote ambaye atakuwa na ajenda nyingine mbali ya kile ambacho kimemleta nchini mwake huku akigusia tuhuma za nchi yake kuwa kinara wa kutoheshimu haki za binadamu.

Ofisi ya wizara ya mambo ya nje za nje ya Uingereza ilitoa taarifa kuwa mbali na kuhudhuria mkutano huo, waziri mkuu Cameron atakuwa na mazungumzo na rais Rajapaksa na atamgusia suala la nchi yake kutuhumiwa kukiuka haki za binadamu na kujaribu kumshawishi kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi kubaini watu waliohusika na mauaji ya wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2009.

Nchi za Canada, India na Mauritiua ziliatangaza hadharani kutotuma mawaziri wake kwenye mkutano huo wakipinga mkutano huo kufanyika nchini Sri Lanka nchi ambayo inatuhumiwa kwakuwa na rekodi mbaya ya kutoheshimu haki za binadamu.

Utawala wa nchi hiyo umesisitiza kuwa ni taifa huru na kwamba hawataruhusu uhuru wao uingiliwe na mtu yeyote hata kama kuna shinikizo toka jumuiya ya kimataifa kuhusu kutakiwa kuruhusu jopo la wachunguzi huru kwenda nchini humo kufanya uchunguzi mpya kuhusu mauaji ya watu zaidi ya elfu 40 wa jamii ya Tamil.

Waziri Cameron mbali na kuwa na mazungumzo na rais Rajapaksa, pia atapata nafasi ya kuonana na familia za watu ambao walipoteza ndugu zao wakati wa vita vilivyodumu kwa zaidi ya miaka 37 nchini humo kabla ya kuhitimishwa mwaka 2009 na jeshi la Serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.