Pata taarifa kuu
INDIA

Watuhumiwa wanne ubakaji nchini India wahukumiwa kunyongwa

Mahakama kuu mjini New Delhi, India, imewahukumu kunyongwa watuhumiwa wanne wa ubakaji ambao juma hili walikutwa na hatia ya kutenda kosa hilo mwezi December mwaka jana.

Waandamanji nchini India wakiwa na mabango kupinga vitendo vya ubakaji na kushinikiza adhabu kali dhidi ya watuhumiwa
Waandamanji nchini India wakiwa na mabango kupinga vitendo vya ubakaji na kushinikiza adhabu kali dhidi ya watuhumiwa Reuters
Matangazo ya kibiashara

Watuhumiwa hao ambao wote kwa pamoja walipatikana na hatia juma hili, wamehukumiwa kunyongwa baada ya majaji kuridhika na ushahidi wa upande wa mashtaka ambao uliita mashahidi zaidi ya mia moja kutoa ushahidi kwenye kesi hiyo.

Hukumu hii ilikuwa inasubiriwa kwa hamu na familia ya msichana ambaye alipoteza maisha kutokana na tukio hilo la ubakaji ambapo msemamji wa familia ameeleza kuridhishwa na hukumu hiyo.

Nchi ya India imekuwa ikishuhudia maandamano makubwa kupinga vitendo vya ubakaji nchini humo ambapo waandamanaji wamekuwa wakishinikiza watuhumiwa wote wanne wahukumiwe kunyongwa.

Awali mwendesha mashtaka wa Serikali aliiomba mahakama iwahukumu kunyongwa watuhumiwa hao kutokana na kosa lenyewe.

Watuhumiwa wote wamepatikana na makosa ya kuteka nyara, ubakaji na mauaji ya kukusudia dhidi ya msichana mmoja aliyekuwa mwanafunzi wa udaktari.

Jaji Yogesh Khanna ndiye aliyesoma hukumu hiyo na kuongeza kuwa hukumu hii ni fundisho kwa watu wengine ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya ubakaji.

Mtuhumiwa mmoja kati ya hao ambaye alikuwa dereva wa basi ambalo watuhumiwa hao walishirikiana kutekeleza kitendo hicho alikutwa amejinyonga kwenye chumba chake cha mahabusu huku mtuhumiwa mwingine akihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.