Pata taarifa kuu
INDIA

Mahakama kuu mjini New Delhi, India yasema inafikiri kuhamisha kesi ya watuhumiwa wa ubakaji nje ya mji huo

Mahakama kuu mjini New Delhi India imesema kuwa italijadili ombi la upande wa utetezi ambao mawakili wao wanataka kesi hiyo isikilizwe nje ya Delhi kwa madai kuwa wateja wao hawatatendewa haki iwapo kesi hiyo itasikilizwa hapo. 

Gari ambalo limetumika kuwabeba watuhumiwa wa ubakaji
Gari ambalo limetumika kuwabeba watuhumiwa wa ubakaji REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Upande wa utetezi umesema kuwa hawaridhishwi na mwenendo wa kesi na kwamba wateja zao hawatatendewa haki iwapo kesi yao ikisikilizwa mjini Delhi na badala yake wameiomba mahakama iamuru kesi hiyo kuhamishwa mjini Delhi.

Kesi ya ubakaji inayowakabili watu watano nchini India inatarajiwa kuendelea kusikilizwa tena hii leo kwenye mahakama moja mjini New Delhi, huku wanaharaati wakiendelea kushinikiza adhabu ya kifo dhidi ya watu hao.

Mtuhumiwa wa sita katika kesi hiyo ambaye ana umri wa miaka 17 pia nae anatarajiwa kupandishwa kizimbani kwenye mahakama maalu ya watoto akikabiliwa na mashtaka ya mauaji, ubakaji na utekaji nyara.

Kesi hiyo imeibua hisia kali miongoni mwa wananchi wa India pamoja na wanaharakati nchini humo ambao wamehoji namna ambavyo wanawake wamekuwa wakitendewa na waume zao bila ya serikali kuwapatia hifadhi.

Mmoja wa mawakili wanaowatetea watuhumiwa hao amesema kuwa hii leo anatarajia kuwasilisha ombi maalumu kwenye mahakama kuu ya Delhi kutaka kesi hiyo ihamishiwe kwenye mahakama nyingine nje ya mji huo.

Wakili huyo ameongeza kuwa sababu ya kutaka kesi hiyo ihamishiwe nje ya mji wa Delhi inatokana na sababu za kiusalama dhidi ya watuhumiwa hao ambao amedai wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya kibaguzi toka kwa wananchi.

Ulinzi mkali umewekwa nje ya mahakama ambako kesi hiyo inasikilizwa huku maelfu ya wananchi wakiwa wamejitokeza nje ya mahakam hiyo wakiwa na mabango ya kuwakashifu watuhumiwa hao pamoja na serikali kwa madai ya kuendelea kuwakumbatia watuhumiwa wa vitendo vya ubakaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.