Pata taarifa kuu
INDIA

Gari Moshi lawaka moto India watu zaidi ya 30 wauawa

Watu zaidi ya 30 wameuawa Kusini mwa India katika mji wa Chennai kwa kuteketea kwa moto baada ya gari moshi walilokuwa wanasafiria kuwaka moto. Mkasa huo umetokea Jumatatu asubuhi wakati gari moshi hilo lilipokuwa linatokea mjini New Delhi na kusababisha abiria wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa na kukimbizwa hospitalini.

Treni ikiteketea kwa moto wakati juhudu za uokozi zikiendelea
Treni ikiteketea kwa moto wakati juhudu za uokozi zikiendelea
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa uokoaji kwa sasa wanaendelea na shughuli za kuwatafuta watu zaidi ambao huenda wamekwama ndani ya gari moshi hilo huku idadi ya wafu ikitarajiwa kuongezeka.

Walioshuhudia mkasa huo wanasema, waliona gari moshi hilo likiwaka moto likiwa safarini, mkasa ambao umeleta kumbukumbuku ya ajali nyingine ya gari moshi iliyotokea mwezi Mei mwaka huu baada ya magari Moshi kugongana na kusababisha zaidi ya watu 20 kuuawa.

Taasisi inayoshughulika na maswala ya ajali za terni nchini humo inasema kuwa tangu mwaka 2009,  watu 25,705 wameuawa kutokana na ajali za gari moshi.

Ajali mbaya zaidi ya gari moshi iliyowahi kuikumba nchi hiyo ilikuwa mwaka 1981 ambapo watu 800 waliuawa baada ya gari moshi la abiria kuzama katika mto katika jimbo la Bihar.

Serikali ya India inasema iko katika harakati za kuimarisha sekta ya safari za reli kwa kuimarisha usalama wa magari moshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.