Pata taarifa kuu
UFARANSA-RWANDA-USHIRKIANO

Wajibu wa Ufaransa nchini Rwanda: Macron aandikia tume

RFI na gazeti "Le Monde", kwa pamoja wamechapisha barua ya kazi iliyotumwa kwa mwanahistoria, raia wa Ufaransa, Vincent Duclert, mwenyekiti wa tume iliyoundwa na Emmanuel Macron kutoa mwanga kuhusu jukumu la Ufaransa wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda.

Wanajeshi wa Ufaransa wakiwasili karibu na mji wa Butare, Rwanda, Julai 3, 1994, siku kumi baada ya koperesheni Turquoise kunza.
Wanajeshi wa Ufaransa wakiwasili karibu na mji wa Butare, Rwanda, Julai 3, 1994, siku kumi baada ya koperesheni Turquoise kunza. HOCINE ZAOURAR / ARCHIVES / AFP
Matangazo ya kibiashara

Miaka ishirini na tano baada ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron siku ya Ijumaa Aprili 5 aliteua kamati ya wataalamu na wanahistoria, ambao watakuwa na kazi ya kuchunguza nyaraka za Ufaransa ili kuweka wazi jukumu sahihi la Ufaransa nchini Rwanda kati ya mwaka 1990 na 1994.

Mapema mwezi Aprili, wanachuoni, walimu na wasomi zaidi ya 280 walitia sahihi kwenye barua inayolaani muundo wa tume hiyo.

Mwanahistoria Vincent Duclert, Inspekta wa Elimu katika ngazi ya taifa, mtaalamu wa elimu ya mauaji ya halaiki, atakuwa mwenyekiti wa tume hiyo. Ameionesha RFI barua aliyotumiwa kutoka ikulu ya Elysée, ambayo ilisainiwa na Emmanuel Macron.

"Natamani kwamba maadhimisho haya ya miaka 25 itakuwa ni fursa kubwa na mafanikio ya kweli ambapo Ufaransa inajifuza na kutoa mafunzo ya mauaji dhidi ya Watutsi, na hali hiyo itabadili taswira na kuelewa maumivu ya waathirika na matarajio ya wale walionusurika katika mauaji hayo," ameandika rais Macron, ambaye ameomba tume alioteua "kukubali ukosoaji wa mwanahistoria kuhusu vyanzo atakavyokuwa ametumia". Kwa lengo hili, wajumbe wa tume hiyo watanufaika kupata kwa urahisi nyaraka kwa ujumla za Ufaransa kuhusu Rwanda kati ya mwaka 1990 na 1994, amebaini Emmanuel Macron.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.