Pata taarifa kuu
MAREKANI-UINGEREZA-TANZANIA-USALAMA

Marekani na Uingereza zaonya raia wao Tanzania

Marekani na Uingereza wametoa wito kwa raia wao waishio nchini Tanzania kuwa waangalifu baada ya polisi kuahidi kuwaadhibu vikali wale watakao jaribu kuitikia wito wa kuandamana dhidi ya serikali.

Wafuasi wa upinzani wakikusanyika mbele ya makao makuu ya chama cha upinzani cha Civic Front United huko Zanzibar mnamo Oktoba 28, baada ya kutangazo la kufutwa kwa uchaguzi.
Wafuasi wa upinzani wakikusanyika mbele ya makao makuu ya chama cha upinzani cha Civic Front United huko Zanzibar mnamo Oktoba 28, baada ya kutangazo la kufutwa kwa uchaguzi. AFP PHOTO / TONY KARUMBA
Matangazo ya kibiashara

Wito huo wa kuandamana dhidi ya John Pombe MAgufuli ulitolewa na wanaharakati wa Tanzania waishio katika nchi za kigeni. Watanzania hao wamewataka raia kuandamana siku ya maadhimisho ya Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar tarehe 26 Aprili 2018. Tanzania Bara na Zanzibar ziliungana Aprili 26, 1964. Wito huo umeonekana kuikera serikali ya Tanzania.

Baadhi ya makamanda wa polisi walisisitiza kuwa wale ambao watathubutu kushiriki maandamano hayo watakiona "cha mtima kuni".

"Polisi inaweza (wakati wa maandamano Alhamisi wiki hii) kutumia mabomu ya machozi, "ofisi ya mambo ya nje ya Uingereza imeonya, huku ikitoa wito kwa raia wa Uingereza waishio nchini Tanzania "kuwa makini "." Maandamano yaliyotangulia yalisababisha vifo. "

Mamlaka ya Uingereza ilipendekeza "kuepuka kuwa karibu na umati wa watu na maandamano", kuwa na "njia ya mawasiliano wakati wote" na kufuatilia maendeleo kupitia vyombo vya habari nchini humo. "

Siku ya Jumanne wiki hii, ubalozi wa Marekani ulitoa onyo kama hilo kwa raia wake waishio Tanzania".

Tayari watu saba wamekamatwa mjini Arusha nchini Tanzania wakihojiwa kuhusiana na majukumu yao katika maandamano ya kisiasa dhidi ya serikali mnamo tarehe 26 Aprili ambayo ni siku ya muungano.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.