Pata taarifa kuu
SIASA-TANZANIA-EU

Umoja wa Ulaya wasikitishwa mauaji yanayokea Tanzania

Umoja wa Ulaya (EU) umetoa tamko la kuelezea wasiwasi wake kuhusu matukio ya mauaji yanayotokea nchini Tanzania na ambayo yanatishia haki za kidemokrasia.

Bendera za nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU).
Bendera za nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU). www.alamy.com-F344F0
Matangazo ya kibiashara

Tamko hilo la Umoja wa Ulaya limetolewa kwa ushirikiano na mabalozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya na kuungwa mkono na mwakilishi na mabalozi wa Norway, Kanada na Uswisi.

“Tunashuhudia kwa wasiwasi mwendelezo wa matukio ya hivi karibuni yanayotishia nidhamu ya demokrasia na haki za watanzania, katika nchi iliyojizolea umaarufu mkubwa duniani kwa utulivu, uhuru na amani,”imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Umoja huo umetaja tukio la karibuni la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Akwilini Akwiline Bafta na kusema unakaribisha wito wa rais wa Tanzania John Magufuli wa uchunguzi wa haraka.

Akwilina Akwiline Bafta alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na aliuawa kwa kupigwa risasi wakati polisi ikitawanya maandamano ya Chama Kikuu cha Upinzani, Chadema. Alizikwa jana wilayani Rombo, Mkoani Kilimanjaro.

Aidha, Umoja wa Ulaya umeelezea wasiwasi wake kuhusu ongezeko la ripoti za ukatili katika miezi ya karibuni ambapo mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wasijulikana na kutoweka kwa mwandishi wa habari wa habari wa gazeti la Mwananchi Azory Gwanda

Matukio mengine yaliyotajwa kwenye taarifa hiyo ni mashambulio yaliyopelekea kupoteza uhai kwa serikali, wawakilishi wa vyombo vya usalama na wananchi yaliyotokea Mkoa wa Pwani ndani ya miaka miaka miwili iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.