Pata taarifa kuu
KENYA-USALAMA

Wanne wauawa Lamu nchini kenya,Alshabab wahusishwa

Watu wanne wameuawa kwa mapanga na nyumba zao kuchomwa moto katika katika kaunti ya Pwani Lamu nchini Kenya,tukio ambalo lawama zinaelekezwa kwa kundi la kiislamu kutoka somalia Alshabab.

Wapiganaji wa kundi la kigaidi la Al Shabab nchini Somalia
Wapiganaji wa kundi la kigaidi la Al Shabab nchini Somalia Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa polisi wa Lamu Larry Kieng amesema wauaji waliwatoa wananchi nje ya nyumba zao na kuwaua,tayari uchunguzi umeanza kubaini kiini cha mauaji hayo.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi watuhumiwa watatu wanashikiliwa na polisi.

Kamanda Kieng amekanusha Alshabab kuhusiska na tukio hilo kwa kile alichodai mauaji hayo yanahusishwa na uhasama kati ya jamii ya wafugaji na wakulima.

Hata hivyo afisa mmoja wa polisi ambaye hakutaka kutaja jina lake ameiambia AFP kuwa shambulizi hilo lina viashiria vya kutekelezwa na wana alshabab.

Hata hivyo kwa mujibu wa shirika la kiintelijensia la SITE wapiganaji wa Alshabab wenye mafungamano na Al Qaeda wamedai kuwaua wakenya watano na kuteketeza nyumba kadhaa katika Pwani ya Kenya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.