Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAZUNGUMZO-SIASA

Mazungmzo ya amani ya Burundi kufanyika wiki hii

Mratibu wa mazungumzo ya amani ya Burundi, rais wa zamani wa Tanzania, Benjamin William Mkapa, ametoa mualiko kwa pande zote zinazokinzana nchini humo, kushiriki kwenye mazungumzo aliyoyaandaa kufanyika juma hili jijini Arusha, nchini Tanzania.

Wakimbizi wa Burundi wakikusanya katika mwambao wa Ziwa Tanganyika katika kijiji cha Kagunga, Kigoma, magharibi mwa Tanzania Mei 17, 2015.
Wakimbizi wa Burundi wakikusanya katika mwambao wa Ziwa Tanganyika katika kijiji cha Kagunga, Kigoma, magharibi mwa Tanzania Mei 17, 2015. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa kwenye mazungumzo ya safari hii ni pamoja na usalama, utawala wa sheria, mkataba wa Arusha, kupanua wigo wa demokrasia nchini Burundi, haki za binadamu na uundwaji wa Serikali ya kitaifa.

Msaidizi wa rais Mkapa, Makocha Tembele, amesema mazungumzo ya tarehe 16 hadi 19 ya mwezi huu, mratibu atatoa tathmini ya kile kilichoafikiwa kwenye mkutano uliopita na kutoa fursa kwa warundi kuzungumza wao kwa wao kufikia suluhu.

Hata hivyo, pamoja na kuwa mwaliko uliotolewa haukwenda moja kwa moja kwa muungano wa CNARED, rais mkapa amewaalika viongozi kutoka kwenye muungano huo, huku swali pakee likiwa ni je serikali ya Burundi itakubali kuketi kwenye meza moja na viongozi hao?

Burundi inakabiliwa na mgogoro wa kisiasa, baaada ya rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula watatu ambapo upinzani unasema ni kinyume na mkataba wa amani wa Arusha.

Mgogoro huo ambao umeingia mwaka wa pili sasa umesababisha maelfu ya raia kuyahama makaazi yao na kukimbilia nchi jirani, huku wato zaidi ya 600 wakisadikiwa kuuawa kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.