Pata taarifa kuu
BURUNDI-UN

UN yatiwa wasiwasi na ukandamizaji dhidi ya mashirika yasio ya kiserikali nchini Burundi

Wiki chache kabla ya kikao kijacho cha Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva mwezi Machi, kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanasema kutiwa wasiwasi, katika ripoti ya ukandamizaji dhidi ya watetezi wa haki za binadamu nchini Burundi.

Jumuiya ya kimataifa yatiwa wasiwasi na Hali ya haki za binadamu nchini Burundi.
Jumuiya ya kimataifa yatiwa wasiwasi na Hali ya haki za binadamu nchini Burundi. © REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimana
Matangazo ya kibiashara

Hali hii si mpya, lakini kwa mtazamo wa wataalamu, hali imekuwa mbaya zaidi katika miezi ya hivi karibuni, ikiwa ni ishara ya nia ya serikali ya Burundi "kuondoa sauti zote pinzani nchini, " kwa mujibu wa wataalamu hao.

Mwandishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu, Michel Forst, ameeleza idadi ya mashirika yasio ya kiserikali ambayo yamepigwa marufuku nchini Burundi. "Mwezi Oktoba, serikali ya Burundi ilifuta mashirika makuu matano yasio ya kiserikali ikiwa ni pamoja na Forsc, Focode na mengineo. Wiki chache baadaye, shirika la haki za binadamu Ligue Iteka, pamoja na Olufad, shirika lingine lisilo la kiserikali vilifutwa kwenye orodha ya mashirika yasio ya kiserikali nchini Burundi. "

Lakini wasiwasi kwa mwakilishi wa Umoja wa Mataifa pia ni hali ya wawakilishi na wanachama wa mashirika hayo. "Tusisahau kwamba viongozi wakuu wa mashirika yasio ya kiserikali wako ukimbizi nje ya nchi, nikimaanisha kwamba walilazimika kukimbilia uhamishoni kutokana na ongezeko la mashambulizi. Wale waliobaki nchini wameendelea kutishiwa usalam wao. Visa vya kukamatwa kiholela, vitisho dhidi yao, vimekua vikiwakabili. "

Muswada wa sheria

Michel Forst amelaani hasa sheria mpya iliyopitishwa na Bunge la Burundi mwezi Desemba mwaka jana, ambayo inaimarisha udhibiti unaotekelezwa na viongozi kuhusu kazi ya mashirika yasio ya kiserikali. "Mwezi Desemba, Bunge lilipitisha miswada miwili yenye lengo la kudhibiti mashirika yasio ya kiserikali, yenye lengo si tu kuzuia, lakini kuyalazimisha mashirika yasio ya kiserikali kuingia katika mfumo walioupanga. "

Mwandishi maalum wa Umoja wa Mataifa ameeleza kwa wasiwasi mkubwa kuhusu nakala hiyo. "Mashirika yasio ya kiserikali yatatakiwa kwanza kupata kibali kutoka Wizara kwa ajili ya shughuli yoyote. Kwa mfano, kuchapisha ripoti, kuanzisha maandamano, inabidi kuomba ruhusa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo inaweza kupinga. "

Udhibiti ambao si tu wa kisiasa, lakini pia kiuchumi. "Mashirika ya sio ya kiserikali pia hayatakiwi kupokea fedha kutoka nje ya nchi, isipokuwa kwa kuomba ruhusa kutoka kwa serikali. "

"Inabidi kuacha mashirika ya kiraia yaseme"

Hatua hizi zote, kwa upande wa Michel Forst, yana lengo moja: kunyamazisha mashirika ya kiraia nchini Burundi. "Huu ni mpango mzima wa uhuru wa msingi, muhimu, ukosoaji, uhuru ambayo vitakosekana muswada huo utapitishwa. Hali hii kwa kweli ni ya machafuko, " amesema Michel Forst.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.