Pata taarifa kuu

Burundi: CNL yataka serikali kupinga kongamano lililomuondoa Rwasa uongozini

Nairobi – Chama kikuu cha upinzani nchini Burundi CNL kimetoa wito kwa viongozi wa juu serikali kupinga kongamano lililoandaliwa mwishoni mwa juma lililopita kumuondoa muasisi wa chama hicho Agathon Rwasa kwenye uongozi.

Agathon Rwasa, kiongozi wa chama cha CNL nchini Burundi.
Agathon Rwasa, kiongozi wa chama cha CNL nchini Burundi. © ONESPHORE NIBIGIRA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliochapishwa hivi majuzi, chama hicho kimemtaka, Rais wa Jamhuri na Waziri Mkuu wa Burundi kutoa maagizo kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ili kutozingatia mahitimisho ya mkutano unaodaiwa kuandaliwa na wapinzani na walioamuwa kujiondowa ndani ya chama cha CNL.

Katibu mkuu wa chama cha CNL Simon Bizimungu amebaini maskitiko yake kwa kuhusika moja kwa moja kwa baadhi ya maafisa wa utawala na wajumbe wa vyombo vya usalama na wa idara ya upelelezi katika kushiriki kwenye kongamano la kejeli na wapinzani na washirika wao kwa niaba ya CNL. Anawataka Mkuu wa Nchi na Waziri Mkuu kuingilia kati ili kukomesha uingiliaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Maendeleo ya Jamii na Usalama wa Umma katika utendaji kazi wa chama cha CNL.

Pia anatoa wito kwa Jukwaa la Vyama vya Siasa kusimamia sheria za nchi na kanuni za vyama vya siasa, huku akiialika jumuiya ya kimataifa pamoja na madhehebu ya dini kufuatilia kwa karibu hali ambayo tayari ni tete ya demokrasia na hali ya sheria nchini Burundi.

Zaidi ya hayo, kundi linalomtii Agathon Rwasa, kiongozi wa kihistoria wa CNL, linapingA kwa nguvu zote matokeo yoyote yanayodhaniwa kuwa ya kongamano lililofanyika katika mji wa Ngozi Jumapili Machi 10, 2024 na "wapinzani ambao wamesimamishwa kutoka kwenye ngazi za uongozi wa chama".

Hayo yanajiri wakati muungano wa vyama vya upinzani kutoka Afrika mashariki ukitoa wito kwa jumuiya ya kikanda na Umoja wa Afrika kufuatilia kwa ukaribu Zaidi hali inayojiri nchini Burundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.