Pata taarifa kuu

DRC: Wanajeshi wa Burundi chini ya EAC wameondoka

Nairobi – Karibia wanajeshi elfu moja wa Burundi chini ya walinda amani wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wameondoka nchini DRC, hatua inayokuja baada ya Kinshasa kukataa kuongeza muda wa vikosi vya EAC mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, jeshi la Burundi limethibitisha.

Wanajeshi wa Burundi wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Goma nchini DRC tarehe 5 ya mwezi Machi 2023.
Wanajeshi wa Burundi wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Goma nchini DRC tarehe 5 ya mwezi Machi 2023. AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati huo ikiwa na wanachama saba, ilituma wanajeshi wake kwa mara ya kwanza mashariki mwa DRC mwezi Novemba mwaka wa 2022 kufuatia wito wa Kinshasa, wakiwa na jukumu la kukomboa vijiji vilivyokuwa vinakaliwa na makundi ya waasi wakiwemo M23.

Kinshasa inasema kuwa wanajeshi wa EAC wameshindwa kutekeleza majukumu waliopewa
Kinshasa inasema kuwa wanajeshi wa EAC wameshindwa kutekeleza majukumu waliopewa AFP - GLODY MURHABAZI

Wanajeshi hao wamekuwa wakituhumiwa na mkuu wa nchi rais Felix Tshisekedi na raia kwenye taifa hilo kwa kushirikiana na makundi ya waasi na kushindwa kurejesha usalama.

Hatua ya wanajeshi wa Burundi kuondoka imekuja baada ya wenzao wa Sudan kusini karibia 250 na wengine 300 wa Kenya kuondoka baada ya muda wao kumalizika siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita.

Msemaji wa jeshi la Burundi, Kanali Floribert Biyereke, amethibitisha kuwasili salama kwa wanajeshi hao wa Burundi katika nchi yao.

Kwa mujibu wa afisa wa ngazi ya juu katika jeshi la Burundi ambaye hakutaka jina lake kutajwa, ameeleza kuwa wanajeshi hao walianza kuondoka nchini DRC siku ya Ijumaa wakitumia malori ya kijeshi yaliopitia katika nchi jirani ya Rwanda kabla ya kuwasili nchini Burundi.

Wanajeshi wa Uganda ambao pia ni sehemu ya EAC, nao pia wanatarajiwa kuondoka nchini DRC katika kipindi cha wiki zijazo.

Wanajeshi wa Kenya pia wameondoka nchini DRC
Wanajeshi wa Kenya pia wameondoka nchini DRC © Alexis Huguet / AFP

Licha ya kuthibitisha kuondoka kwa wanajeshi wa Burundi, msemaji wa jehsi hilo alikataa kuzungumzia kuhusu maofisa wake wengine ambao wanagali nchini DRC kwa makubaliano ya Kinshasa na Bujumbura.

Serikali ya DRC pia imewakubalia wanajeshi wa Uganda kuwasaka waasi wa ADF mashariki mwa taifa hilo.

Waasi wa ADF kihistoria wanatokea nchini Uganda na waliingia nchini DRC katika miaka ya 1990 ambapo wanahusishwa na kundi la wapiganaji wa Islamic State.

Makundi ya waasi ikiwemo ADF na M23 wamekuwa wakiendelea kutekeleza mashambulio dhidi ya raia wa mashariki mwa DRC
Makundi ya waasi ikiwemo ADF na M23 wamekuwa wakiendelea kutekeleza mashambulio dhidi ya raia wa mashariki mwa DRC AP - Jerome Delay

Serikali ya DRC na mataifa kadhaa ya Magahribi yanasema waasi wa M23 wanaungwa mkono na nchi jirani ya Rwanda licha ya Kigali kupinga tuhuma hizo.

Rais Tshisekedi, ambaye aliingia madarakani mwaka wa 2019 baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata, anawania kwa muhula wa pili katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 20 ya mwezi Desemba.

DRC imekuwa ikiituhumu jirani yake Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 suala ambalo kigali imeendelea kukana
DRC imekuwa ikiituhumu jirani yake Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 suala ambalo kigali imeendelea kukana © AFP - SIMON WOHLFAHRT

Mkuu wa nchi ameahidi kuboresha maisha watu wanaoishi katika umaskini, kupiga vita ufisadi pamoja na kumaliza utovu wa usalama mashariki mwa nchi.

Kutokana na uasi wa M23, uchaguzi hautofanyika katika maeneo ya Masisi na Rutshuru katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.