Pata taarifa kuu

Mahakama ya juu Kenya yaidhinisha ushindi wa William Ruto

Mahakama ya Juu nchini Kenya, imetupilia mbali pingamizi la mwanasiasa wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, kupitia muungano wa kisiasa wa Azimio, ambao ulikuwa unapinga ushindi wa William Ruto. Uamuzi wa Majaji ulikuwa ni wa Jumla ulioungwa mkono na wote. Ndani ya siku 21 uamuzi kamili kutolewa.

Wafuasi wa William Ruto wakisherehekea ushindi wake mjini Eldoret, Jumatatu hii Agosti 15, 2022.
Wafuasi wa William Ruto wakisherehekea ushindi wake mjini Eldoret, Jumatatu hii Agosti 15, 2022. AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya juu imeidhinisha Uchaguzi wa William Ruto kuwa rais mteule wa Kenya. Majaji wakioongozwa na jaji mkuu Martha Koome walisema kwamba ushahidi uliotolewa na mlalamishi Raila Odinga ulikuwa umejaa uvumi na porojo.

Jaji Martha Koome amesema kuwa mshindi wa uchaguzi huo William Ruto alifanikiwa kupita kikwazo cha kura asilimia 51 ya kikatiba, huku akiongeza kwamba mbinu iliotumika na tume ya uchaguzi kupata asilimia 64.4 ya wapiga kura ilikuwa sahihi.

Jaji Koome amesema hakukuwa na ushahidi kwamba fomu za uchaguzi katika tovuti ya matokeo ya mtandaoni zilibadilishwa kutoka fomu za awali zilizochapishwa.

Mnamo Agosti 15, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ilimtangaza Dkt Ruto kuwa Rais mteule baada ya kupata kura milioni 7,176,141 aliyepata asilimia 50.49 dhidi ya milioni 6,942,930 za Bw Odinga, ambaye alipata asilimia 48.85).

Raila Odinga aliwasilisha mahakamani malalamiko yake akibaini kwamba kura hiyo ilibadilishwa ili kumpa mpinzani wake William Ruto ushindi mwembamba katika uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.