Pata taarifa kuu

Uchaguzi Kenya: Kampeni zagubikwa na 'habari za uwongo'

Siku moja kabla ya uchaguzi wa urais nchini Kenya habari za uongo zimeendelea nafasi ya mbele katika kampeni za uchaguzi. Wakenya milioni 22 wanajiandaa kupiga kura Jumanne Agosti 9 kumchagua mrithi wa Uhuru Kenyatta. Kampeni iliyomalizika kwa ujumla ilikuwa ya amani, lakini ziligubikwa na kuenea kwa "habari za uwongo", kwenye mitandao ya kijamii kwa wakati mwingine zikiwa na matamshi ya chuki.

Mitandao ya kijamii inayotumiwa kwa kusambaza "habari za uongo" ni Twitter na Facebook, lakini pia programu ya TikTok.
Mitandao ya kijamii inayotumiwa kwa kusambaza "habari za uongo" ni Twitter na Facebook, lakini pia programu ya TikTok. AFP - OLIVIER DOULIERY
Matangazo ya kibiashara

Kilichotawala katika kampeni za urais ni jumbe zinazowashutumu wagombea wawili wakuu (William Ruto na Raila Odinga) kwa kujiandaa kuvuruga uchaguzi. Taarifa za uwongo zinazolenga kuhalalisha matokeo ya uchaguzi. Lakini pia kumekuwa kukionekana kwa wiki kadhaa utabiri wa uwongo kuhusiana na matokeo ya uchaguzi, kulingana na picha zilizopigwa, na video zilizorikodiwa, ambazo baadhi yake zina vitisho vya wazi vinavyolenga jumii moja au nyingine. Pia kwenye video hizo kunasikika hotuba fupi inayodaiwa kuwa ni ya William Ruto, yenye kichwa: "Ruto anachukia Wakikuyu [jamii kuu nchini Kenya] na anataka kulipiza kisasi". Video ilikuwa imetengenezwa kwa kupaka matope William Ruto.

Mitandao ya kijamii inayotumiwa kwa kusambaza "habari za uongo" ni Twitter na Facebook, lakini pia programu ya TikTok. Katika ripoti iliyochapishwa mwezi Juni, mtafiti kutoka Wakfu wa Mozilla anadai kuwa aliona video 130 za habari zisizo za kweli kwenye TikTok, wakati mwingine zenye maudhui ya vurugu, zilizotazamwa zaidi ya mara milioni 4 nchini Kenya, ambayo bila shaka ni sampuli tu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.