Kenya: Hatutazima Facebook wakati wa uchaguzi: Waziri Joe Mucheru
Waziri wa masuala ya mawasiliano na teknolijia nchini Kenya, Joe Mucheru, ametupilia mbali uwezekano wa kuufungia mtandao wakijamii wa facebook wakati wa uchaguzi mkuu wa Agosti 9.
Imechapishwa:
Matamshi yake yanakinzana na yale yaliyotolewa na tume ya maridhiano na utangamano, ambayo ilisema inatoa siku 7 kuanzia jana kwa kampuni ya facebook kudhibiti lugha za uchochezi na chuki zinazochapishwa kwenye mtandao wake.
Waziri Mucheru hata hivyo anasema serikali imejipanga kuhakikisha uhuru wa watu kutoa maoni unaheshimiwa na kwamba haitajihusisha na kutoa vitisho vya kuufungia mtandao huo.
Kauli yake ikijaribu kuzima hofu iliyokuwepo miongoni mwa washika dau kuwa, Serikali inapanga kuzima huduma ya mitandao ya kijamii wakati wa uchaguzi wa Agosti 9, akisisitiza kutofungiwa kwa mtandao wowote wala huduma ya Internet.
Kwa mujibu wa tume ya utangamano na maridhiano, mtandao wa Facebook umeshindwa kuchuja arafa za chuki na uchochezi, hali inayotishia kusababisha vurugu.