Pata taarifa kuu
Kenya - Siasa

Kenya : Raila Odinga aapa kukabili rushwa iwapo atachaguliwa

Mgombea urais kupitia muungano wa Azimio la Umoja, One Kenya Raila Odinga amesema ana uhakika wa kushinda uchaguzi utakaofanyika tarehe tisa mwezi ujao.

Mgombea urais nchini Kenya, Raila Odinga
Mgombea urais nchini Kenya, Raila Odinga © Raila Odinga twitter
Matangazo ya kibiashara

Odinga, anayewania uongozi wa nchi hiyo kwa mara tano sasa, akizungumza na wanahabari wa Kimataifa jijini Nairobi wiki hii, hata hivyo amesema atakubali matokeo iwapo uchaguzi utakuwa wa haki na kuwataka wapinzani wake pia kufanya hivyo.

Tumesema kama wagombea wa  Azimio kuwa, iwapo tutapoteza kwa haki, tutakubali matokeo na kumpongeza mshindi, tunamaanisha hili , na tunaomba wapinzani wetu wawe tayari kukubali matokeo ya uchaguzi huu.

Waziri Mkuu huyo wa zamani pia, anaitaka Tume ya uchaguzi kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unakuwa huru na haki kwa ajili ya amani ya nchi.

Raila amesema  kwamba raia wa Kenya ni watu wanaopenda amani, changamoto  ni tume ya uchaguzi kuhakikisha kuwa uchaguzi unakuwa huru na haki, na iwapo tume itahakikisha hilo kuanzia upigaji kura, hadi ujumuishwaji wa  matokeo, hakuna haja ya kuwa na wasiwasi, ana uhakika watu watakubali matokeo.

Iwapo atachukua hatamu za uongozi wa nchi hiyo, Odinga ameapa kupambana na rushwa,hata kama atakuwa mtoto wake, kakake au dadake , wakipatikana wamehusika na rushwa, watakabiliwa na sheria, na kuongeze kuwa wakati umefika wa kulikabili suala hili kwa nguvu kwa sababu limekuwa kama saratani kwenye jamii, Odinga akiapa  kuwa atapambana na janga hilo, bila kuogopa.

Kuhusu kupanda kwa gharama ya maisha, mgombea huyo pia ameahidi kufanya mageuzi itakayosaidia kushuka kwa bei ya vyakula akiaminikuwa  asuluhisha suala hilo kwa sababu amewahi kuhudumu serikalini, na atafanikiwa tutakabiliana na uhaba wa chakula na kupanda kwa gharama ya maisha, kwa kufanya mageuzi muhimu .

Amepinga kauli za wapinzani wake, ambao wamekuwa wakisema yeye ni mradi wa kisiasa wa rais anayemaliza muda wake Uhuru Kenyatta.

Ukweli ni kwamba Wakenya wanafahamu na hawawezi kukubali hiyo proapaganda wananifahamu vema kuwa mimi nina misimamo na siwezi kuwa kibaraka au mradi wa mtu, kile ambacho hawasemi hawa wapinzani wetu  ilikuwaje tukakubaliana kufanya kazi na rais anayeondoka madarakani  Uhuru Kenyatta,

amesema Odinga

Odinga mwenye umri wa miaka 77, amekuwa akisema aliamua kuwania uongozi wa nchi hiyo kufuatia shinikizo 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.