Pata taarifa kuu
KENYA- SIASA

Uhuru Kenyatta : Martha Karua atawafunga jela wanasiasa wezi.

Nchini kenya wakati huu ambapo kampenzi za uchaguzi mkuu wa mwezi agosti zinapoendelea kushika kasi, rais Uhuru Kenyatta anayemaliza muhula wake ameonya kuwa watu anaowataka wamrithi watawafunga jela wanasiasa wote wafisadi.

Raila Odinga na mgombea mwenza wake Martha Karua.
Raila Odinga na mgombea mwenza wake Martha Karua. AFP - TONY KARUMBA
Matangazo ya kibiashara

Bila kutaja aliokuwa anwalenga katika usemi wake, wachambuzi wa siasa kwenye taifa hilo la Afrika mashariki wanasema kuwa maneno yake Kenyatta yalikuwa yanamlenga naibu William Ruto na mrengo wake wa Kenya kwanza.

Rais Kenyatta ambaye wachambuzi wa siasa wametaja kama kiongozi mpole na mwepesi wa kabiliana na madui zake, ametaja kuwa serikali ya Azimio la Umoja yake waziri mkuu wa zamani Raila Odinga na aliyekuwa kwa wakati moja waziri wa masuala ya sheria na haki  Martha Karua haitawasamehe wafisadi kama ambavyo amekuwa akifanya katika utawala wake wa miaka 10.

Uhuru aidha ametumia wakati huo kuwaomba wakaaji wa jiji la Nairobi kupigia kura mrengo wa Azimio, Kenyatta akisema kuwa anamatumaini makubwa kwamba wakenya watampigia Odinga ili amkabidhi madaraka baada ya uchaguzi wa agosti 9.

Odinga, rais, akieleza kuwa ndiye kiongozi peke aliye na uwezo wa kuedeleza miradi yote ya serikali iliyoaanzishwa na utawala wake atakapondoka ofisini.

 “Ninawaomba kwa heshima muunge mkono mtu ambaye ntawakabidhi, na hatakuwa mwengine japokuwa Raila Odinga kwa sababiu kazi ambayo tumeifanya itashugulikwa” Rais Kenyatta.

“Ninaona uwongozi wa Raila na Karua kama bora kwa taifa letu. Ukweli usemwe. Ule mrengo mwengine unazungumza tu mambo yasio na maana na matusi. Wanapoenda katika mikutano  ya kisiasa kila mtu ni kunitaja tu ilihali mimi sigombea mahali popote,” alisema Kenyatta.

Aidha rais alisema kuwa Odinga atalileta taifa pamoja pasipo na kuwa na tama ya kuangalia masilahi yake, iliganishwa na viongozi wengine ambao amewataja kutokuwa na nia ya kuwalinda raia.

Rais vile vile amewataka wakaazi wa Nairobi kutopigia kura mrengo wake naibu rais Ruto kwa madai kuwa wote wanania ya kuwagawa wakenya kwa misingi ya uchochezi badala ya kuangazia matatizo yanayowakumba wakenya.

Kenyatta amemkashifu naibu wake Ruto na wandani wake ambao katika mikutano yao ya kisiasa wamesikika wakimwambia amalize hatamu yake kisha aende nyumbani, akisema kuwa atakuwepo hadi pale ambapo atapeana uwongozi kwa serikali mpya baada ya uchaguzi mwa agosti 9.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.