Pata taarifa kuu
Ethiopia - Usalama

Ethiopia : Amnesty yashinikiza uchuguzi wa mauwaji ya raia 400

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty, linaitaka serikali ya Ethiopia, kuendesha uchuguzi kuhusiana na mauwaji ya kikabila ya raia zaidi 400, yaliofanyika katika eneo la Oromia.

Picha Shirika ya kutetea haki za binadamu la Amnesty International
Picha Shirika ya kutetea haki za binadamu la Amnesty International @សហការី
Matangazo ya kibiashara

Amnesty International limeyataja mauwaji hayo kuwa ya kutisha, kutokana na kwamba mauwaji mengine ya yalitekelezwa katika wilaya tofauti eneo hilo.

Vurugu hizo zilizoshuhudiwa katika wilaya za Tole na Gimbi zilielekezwa dhidi ya raia wakulima eneo la Amhara.

Kundi la watu wenye silaha la Oromo Liberation Army (OLA), linatuhumiwa kuhusika kwa mauwaji hayo, serikali ikikosolewa kwa kukosa kuwakabili wahusika wa mauwaji hayo.

Mashuhuda wanasema vikosi vya serikali viliwasili muda mrefu baada ya washumbuliaji hao kuondoka.

Hata hivyo kundi la OLA, limekanusha kuhusika kwa mauwaji hayo likituhumu kundi ambalo linadai linafadhiliwa na serikali.

Serikali ya Ethiopia ilikuwa imeahidi kuendesha uchuguzi na kuwachukulia wahusika hatua, ila raia wengi eneo hilo wametia shaka uchuguzi huo wa serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.