Pata taarifa kuu
Ethiopia - Usalama

Ethiopia : Serikali yatangaza kutekelezwa kwa hali ya dharura Gambella

Serikali ya Ethiopia imetangaza kutekelezwa kwa hali ya dharura katika jiji la Gambella, magharibi mwa taifa hilo, ikiwa na hatua ya serikali kujaribu kumaliza hali ya utovu wa usalama ambayo imekuwa ikishuhudiwa katika jiji hilo.

Mwanachama wa wapiganaji wa  Amhara akiwa ameshikilia bunduki yake huku mwingine akinawa uso wake huko Humera, Ethiopia mnamo tarehe 22 Novemba.
Mwanachama wa wapiganaji wa Amhara akiwa ameshikilia bunduki yake huku mwingine akinawa uso wake huko Humera, Ethiopia mnamo tarehe 22 Novemba. © AFP - Eduardo Soteras
Matangazo ya kibiashara

Hali hiyo ya dharura inazuia raia kutembea nyakati za saa mbili jioni hadi saa kumi na moja alfajiri.

Jiji la Gambella lilishuhudia mapigano makali mwezi uliopita kati ya vikosi vya serikali na makundi ya watu wenye silaha ya Oromo Liberation Army (OLA)  na lile la Gambella Liberation Front, ambayo yalikuwa yamechukuwa udhibiti wa jiji hilo kwa saa kadhaa, kabla ya wanajeshi wa serikali kulikomboa, zaidi ya raia 40 wakidaiwa kupoteza maisha.

Serikali ya Ethiopia pia inatekeleza hali ya dharura, katika eneo la Assosa, jiji la Benishangul-Gumuz, tangu mapema mwezi uliopita.

Maeneo la magharibi mwa Ethiopia, limekuwa likishuhudia vurugu kwa miezi kadhaa sasa, raia wakiropitiwa kuuawa na jamii ndogondogo zikilengwa na makundi ya watu wenye silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.