Pata taarifa kuu
Kenya - Siasa

Kenya: Wagombea wenza wa urais washiriki mdahalo

Nchini Kenya, usiku wa kuamkia leo kumefanyika mdahalo wa wagombea wenza wa urais, kuelekea uchaguzi Mkuu utakayofanyika tarehe tisa mwezi ujao.

Martha Karua kushoto, mgombea mwenza wa Raila Odinga na Rigathi Gachagua, kulia mgombea mwenza wa william Ruto
Martha Karua kushoto, mgombea mwenza wa Raila Odinga na Rigathi Gachagua, kulia mgombea mwenza wa william Ruto © Martha karua
Matangazo ya kibiashara

Wagombea wenza wanne, walipambana katika mdahalo huo kueleza agenda zao kuwarai wapiga kura kuwapigia kura.

Mbali na Ruth Mutua na  Justina Wamae,  macho na masikio yalielekezwa kwa Martha Karua na Rigathi Gachagua wanaopewa nafasi kubwa katika uchaguzi huu.

Miongoni mwa maswala waliolizwa ni kuhusu ni vipi watakabiliana na rushwa, Karua ambaye ni mgombea mwenza wa Raila Odinga akisisitiza kwamba serikali ya Raila Odinga itapambana wafisadi na kuahidi kuboresha maisha ya wakenya.

Karua anasema lengo kuu la serikali ya Odinga ni kuleta ukombizi wa tatu wa taifa hilo utakaohusisha uchumi.

Naye, Gachagua mgombea mwenza wa William Ruto alieleza mpango wa muungano wake wa Kenya Kwanza, ambapo ameeleza mpango wao wa kuhakikisha wakenya wa kaida wananufaika na miradi mbalimbali ya serikali.

Juma lijalo, kutakuwa na mdahalo mwingine, ambao utawakutanisha wagombea urais wanne, wanaotaka uongozi wa nchi hiyo, akiwemo naibu rais William Ruto na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.