Pata taarifa kuu
Kenya - Siasa

Odinga aongoza kwa umaarufu nchini Kenya

Umaarufu wa kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, umeongezeka kwa asilimia tatu na kufikia asilimia 39 dhidi ya mpinzani wake mkuu naibu rais wa taifa hilo, William Ruto, ambaye umaarufu wake umepungua  kutoka asilimia 39 na kufikia asilimia 35

Raila Odinga kiongozi wa upinzani nchini Kenya, pamoja na Naibu rais William Ruto
Raila Odinga kiongozi wa upinzani nchini Kenya, pamoja na Naibu rais William Ruto © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mjibu wa shirika la utafiti la TIFA, umaarufu wa Odinga umeongezeka kutokana na hatua yake kumteua mgombea mwenza wa kike, ambaye alikuwa waziri wa haki Martha Karua.

Utafiti huo ulihusisha wakenya 1, 719 ambao waliohojiwa kupitia njia ya simu.

Odinga ambaye aliwahi kuhudumu kama waziri mkuu nchini Kenya, katika kura ya maoni ya mwezi April, alikuwa na asilimia 32 ya umaarufu dhidi ya Ruto aliyekuwa na asilimia 38.

TIFA katika utafiti wao pia wamebaini kuwa chama cha naibu rais Ruto, UDA, kinaongoza kwa umaarufu kwa asimilia 29 dhidi ya kile cha Odinga kwa asilimia 25.

Uchaguzi wa urais nchini Kenya, unatarajiwa kufanyika Agosti 9 mwaka huu, kipindi cha kampeini kikitarajiwa kuanza mwisho wa mwezi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.