Pata taarifa kuu
Kenya - Siasa

Kenya: Martha Karua ateuliwa kuwa mgombea mwenza wa Odinga

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, amemchagua kiongozi wa chama cha Narc Kenya, Martha Karua, kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi unaotarajiwa mwezi agosti.

Martha Karua mgombea mwenza wa  Odinga nchini Kenya
Martha Karua mgombea mwenza wa Odinga nchini Kenya © Marha Karua
Matangazo ya kibiashara

Karua anakuwa mwanamke kwanza kuteuliwa kuwa mgombea mwenza chini ya katiba ya mwaka 2010.

Odinga amesifia juhudi za Karua kupigania haki za binadamu nchini humo, pamoja na kuhakikisha sheria zinangatiwa.

Chagua la Karua limesabisha mganyiko ndani ya muungano wa Azimio unaongozwa na Odinga na rais Uhuru Kenyatta, baada ya jina la aliyekuwa makamo rais Kalonzo Musyoka kuwaachwa nje.

Katika mkutano mwingine tofauti, Musyoka amemtakia Karua kila la heri, akisema tayari wameskizana na Odinga kwamba hawatakuwa pamoja, licha ya Odinga kusema kwamba atahudumu kama kiongozi wa shughuli za serikali bungeni iwapo ataibuka mshindi kwenye uchaguzi wa agosti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.