Pata taarifa kuu
BURUNDI-UNSC

UNSC inatiwa hofu na mvutano unaoendelea Burundi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea jana wasiwasi wake kuhusu mvutano wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi wakati ambapo nchi hiyo inajiandaa kwa uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Samantha Power akizungumza jinsi hali ilivyo nchini Burudi
Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Samantha Power akizungumza jinsi hali ilivyo nchini Burudi REUTERS/Eduardo Munoz
Matangazo ya kibiashara

Wakati huohuo wajumbe 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wameelezea jana mbele ya baraza hilo wasiwasi wao juu ya mvutano wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi, rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Joy Ogwu, ambaye ni balozi wa Nigeria kwenye baraza hilo, ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Newyork.

Naibu katibu wa Umoja wa Mataifa anehusika na masuala ya siasa, Jeffrey Feltman.
Naibu katibu wa Umoja wa Mataifa anehusika na masuala ya siasa, Jeffrey Feltman. Reuters

Naibu katibu wa Umoja wa Mataifa anaehusika na masuala ya siasa, Jeffrey Feltman, ameelezea wajumbe hao wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hali inayojiri nchini Burundi, na kubaini kwamba hali itaendelea kuwa mbaya kutokana na uhasama unaojitokeza mara kwa mara kati ya vijana kutoka vyama vya kisiasa. Ameiomba jumuiya ya kimataifa kuitoingilia kati ikihitajika.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa pande zote husika kuketi kwenye meza ya mazungumzo bila kumtenga yeyote, mazungumzo ambayo yatajikita kwenye mkataba uliyoafikiwa na tabaka zote za warundi mjini Arusha, nchini Tanzania mwaka wa 2000.

Hayo yakijiri, balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Samantha Power, amefanya ziara fupi nchini Burundi na kukutana kwa muda wa masaa mawili na Rais Pierre Nkurunziza ambaye ameletewa ujumbe kutoka kwa rais wa Marekani Barack Obama.

Bi Power amefahamisha kwamba amekutana na rais Nkurunziza na kumuonyesha hali ya wasiwasi mbaya Marekani inayo kuhusu hatma ya Burundi.

“Tumekuwa na mazungumzo ya wazi sana na Rais Nkurunziza. Tumezungumzia hatua ya maendeleo iliyofikiwa na nchi ya Burundi lakini pia wasiwasi uliopo kuhusu uhuru wa kujieleza, na kukusanyika pamoja na katiba ya nchi zikiwemo haki zote ambazo lazima ziheshimiwe, kwa hiyo tumesisitiza kuwa Katiba ya nchi, ambayo ni sheria mama na Haki za binadamu viheshimiwe”, amesema Samantha Power.

Nchi ya Burundi inajiandaa katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2015, mvutano wa kisiasa ukiendelea kushuhudiwa kwa majuma kadhaa, mvutano ambao umetokana na kujiondoa kwa chama cha UPRONA (chenye wafuasi wengi kutoka jamii ya watutsi) serikalini inayoongozwa kwa sehemu kubwa na watu kutoka jamii ya wahutu kutoka chama cha CNDD-FDD, kiliyokua zamani chama cha waasi.

Mvutano huo wa kisiasa uleshika kasi pale tu kulikotokea makabiliano makali kati ya vijana wafuasi wa chama cha upinzani cha MSD na polisi, machi 8 mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.