Pata taarifa kuu
BURUNDI-Siasa

Chama cha upinzani cha MSD nchini Burundi chafungiwa shughuli zake kwa miezi minne

Chama cha upinzani cha MSD nchini Burundi kimefungiwa kwa kile serikali inasema imehusika na uausi na kuchochea chuki na vurugu nchini humo, huku kukiwa na hali mbaya ya mvutano katika taifa hilo dogo la Afrika ya kati. Hatua hiyo imechukuliwa na waziri wa mambo ya ndani, Edouard Nduwimana.

WAziri wa mambo ya ndani wa Burundi edouard Nduwimana
WAziri wa mambo ya ndani wa Burundi edouard Nduwimana RFI
Matangazo ya kibiashara

Bujumbura inasema vurugu za juma lililopita zimechangia kufungiwa kwa chama hicho ambacho wafuasi wake walikabiliana na maafisa wa usalama na kusababisha wafusi wao zaidi ya sabini kutiwa nguvuni na kufungiliwa mashtaka akiwemo kiongozi wa chama hicho Alexis Sinduhije.

Katika makabiliano hayo watu 20 wakiwemo askari polisi 5 walijeruhiwa kwa risase.
Thierry Vircoulon, muakilishi Maalum wa Shirika la Kimataifa la kuangazia mizozo ya Kimataifa la International Crisis Group katika Ukanda wa maziwa Makuu ameinyooshea kidole cha lawama serikali ya Burundi kwamba nia yake ni kuwafanyia vitisho na kuwabana wanasiasa wa upinzani.

“Kwa kweli Huu ni mfumo ambao unaashiria kwamba chaguzi zitakazofanyika mwakani pamoja na maandalizi kwa upande wa Upinzani vinaweza vikawa na Ugumu fulani, na nafikiri kuwa serikali inajaribu kuwabana wanasiasa nchini Burundi, tukizingatia kwamba mwaka 2014 ni mwaka wa kujiandaa kwa chaguzi”, amesema Vircoulon .

Awali Muungano wa vyama vya upinzani ADC-Ikibiri ulinyooshea kidole utawala wa Pierre Nkurunziza kwamba una lengo la kuwabana wanasiasa wa upinzani kwa madai ya kubadili katiba bila kuwashirikisha wanasiasa wote, wakiwemo wale kutoka vyama vya upinzani.

Hivi karibuni, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton, Marekani, na ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi (BNUB) wamelani vikali makabiliano kati ya wafuasi wa chama cha MSD na polisi yaliyotokea machi 8 mwaka huu, na mwenendo wa polisi wa kutumia nguvu dhidi ya upinzani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.