Pata taarifa kuu
INDIA-Uchaguzi

Uchaguzi mkuu wafanyika India

Raia nchini India hii leo wameanza kupiga kura kwenye uchaguzi unaotajwa kuwa mkubwa zaidi duniani, huku chama tawala nchini humo cha Congress kikitarajiwa kupata upinzani toka kwa vyama vya upinzani. 

Kituo cha kupigia kura nchini India, aprili 7 mwaka 2014.
Kituo cha kupigia kura nchini India, aprili 7 mwaka 2014. Adnan Abidi/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu ambao utafanyika kwa awamu tisa tofauti, unatarajiwa kukamilika tarahe 12 ya mwezi May mwaka huu, huku kura zikitarajiwa kuanza kuhesabiwa tarehe 16 ya mwezi May baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika.

Zaidi ya wananchi milioni nane wamejiandikisha kushiriki kwenye uchaguzi huu, uchaguzi ambao umegubikwa na mazingira ya rushwa ambapo suala hilo linatarajiwa kuwa sehemu ya maamuzi ya wananchi kuchagua chama ambacho wanaona kitaleta mabadiliko.

Kutokana na ukubwa wa uchaguzi wenyewe, wachambuzi wa mambo wanadai kuwa haitakuwa rahisi kwa chama kimoja peke yake kushinda kwenye uchaguzi huo na badala yake vitalazimika kuunda muungano ambao utawawezesha kupata wingi wa kura zinazohitajika kutangazwa kuwa mshindi.

Chama tawala cha Congress kinatarajiwa kupata upinzani mkali toka kwa chama kikuu cha upinzani cha Hindu Nationalist BJP pamoja na chama kipya kinachopinga rushwa nchini humo cha AAP, ambavyo vyote kwa pamoja vinapewa nafasi kubwa ya kutwaa viti vingi vya ubunge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.