Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-Uchaguzi

Afghanistan yashuhudia uchaguzi wa kihistoria licha ya tishio la mashambulizi ya kigaidi

Wapiga kura nchini Afghanstan wameanza zoezi la kupiga kura ya kuchagua raisi mpya uchaguzi ambao unakuwa wa kihistoria kwa taifa hilo kubadili utawala kwa njia ya kupiga kura.

Askari walinzi wa usalama
Askari walinzi wa usalama REUTERS/Mohammad Ismail
Matangazo ya kibiashara

Zoezi hilo linafanyika chini ya operesheni kubwa ya kiusalama inayofanywa na majeshi ya taifa hilo ili kuwalinda wapiga kura na maafisa uchaguzi, baada ya kundi la Taliban kuapa kuvuruga uchaguzi huo wa hii leo.

Wagombea nane wanashiriki katika kinya'nganyiro hicho ili kukalia kiti cha raisi anayemaliza muda wake Hamid Karzai ambaye Katiba ya nchi hiyo ilimzuia kuwania kwa awamu ya tatu mfululizo.

Hata hivyo maandalizi ya Uchaguzi huo yaligubikwa na mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari wawili ambapo mmoja alipoteza maisha.

 Wanahabari hao walishambuliwa ndani ya gari yao katika wilaya ya Tanai jimboni Khost mashariki mwa nchi hiyo wakati wakiripoti kuhusu ugawaji wa karatasi za kupigia kura kwa ajili ya uchaguzi kumtafuta mrithi wa rais Hamid Karzai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.