Pata taarifa kuu
BURUNDI-Siasa

Burundi: Rais wa chama cha upinzani cha MSD, Aléxis Sinduhije atafutwa kwa udi na uvumba

Vyombo vya sheria nchini Burundi vimemfungulia mashitaka kiongozi wa chama cha MSD, Aléxis Sinduhije, pamoja na wafuasi 71 wa chama hicho wakituhumiwa kuhamasisha watu kuanzisha vurugu dhidi ya utawala, kosa ambalo hukumu yake, ni kifungo cha maisha jela.

Aléxis Sinduhije, rais wa chama cha upinzani cha MSD, akiwahutubia wafuasi wake.
Aléxis Sinduhije, rais wa chama cha upinzani cha MSD, akiwahutubia wafuasi wake. RFI
Matangazo ya kibiashara

Tuhuma hizo zinakuja baada ya makabiliano mabaya kushuhudiwa nchini humo baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 kati ya wafuasi wa chama cha MSD na polisi, na hali hio inaweza ikahatarisha hali kuwa mbaya katika taifa la Burundi, ambalo lilitoka katika vita vya wenyewe kwa wenyewe katika mwaka wa 2006, vita ambavyo vilidumu zaidi ya miaka kumi.

Wafuasi 71 wachama cha MSD, waliyokamatwa jumamosi katika makabiliano na polisi,wanaziwiliwa, huku hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa chama cha MSD, Aléxis Sinduhije, ikiwa imetolewa.

Mwanahabari huyo wazamani, akiwa pia muanzilishi wa kituo cha redio ya umma (RPA), moja ya redio za kibinafsi zinazosikilizwa sana nchini Burundi,alirudi nchini yapata mwaka moja, baada kukimbilia uhamishoni kwa hofu ya kukamatwa, akituhumiwa kumiliki kundi la wapiganaji.

Wafuasi wa chama cha MSD, ambao walikua katika “mazowezi ya kunyoosha misuli”, katikati mwa mji wa Bujumbura, walitawanywa na polisi ikitumia mabomu ya kutoa machozi.

Takribani wafuasi 200 walikimbilia katika makao makuu ya chama cha MSD, na kuwateka askari polisi wawili, kabla ya polisi kuanza kushambulia wafuasi hao.

Makabiliano ahyo yalidumu zaidi ya saa moja, na kusababisha wafuasi 20 kujeruhiwa kwa risase, wakiwemo askari polisi watanu. Polisi imekuwa ikiwatuhumu wafuasi wa chama cha MSD kwamba wao ndio walianza kufyatulia risase askari polisi.

“Tumewafungulia mashitaka watu 71, waliyokamatwa jumamosi, tukiwatuhumu uasi, ukaidi na machafuko dhidi ya polisi na kuanzisha uasi”, kiongozi wa mashitaka katika manispa ya Bujumbura Arcade Nimubona ameliambia shirika la habari la AFP.

Hati ya kukamatwa dhidi Aléxis Sinduhije, ambaye yuko ukimbizini, imetolewa, akituhumiwa “kushiriki katika kundi lililoanzisha vurugu likitumia silaha”, ameendelea kusema afisa huyo, akibaini kwamba ana matumaini ya kuanza haraka kwa “kesi hio”.

 

Chama cha MSD, kiliundwa mwaka 2009, na ni moja kati ya vyama vigogo vya upinzani, na wengi wa wafuasi wa chama hicho ni vijana. Chama hicho kilijiondoa katika uchaguzi wa madiwani uliyofanyika mwichoni mwa mwezi mei mwaka 2010, na kususia chaguzi ziliyofuata, ziliyopelekea chama cha CNDD-FDD kuibuka mshindi.Wakati huohuo, mkuu wa sera za nje wa umoja wa Ulaya, Catherine Ashton, amesema jana kwamba anatiwa wasiwasi na hali ya kisiasa inayoendelea nchini Burundi, huku akizitaka pande zote husika kuketi kwenye meza ya mazungumzo.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi (BNUB), imebaini kwamba matukio yaliyotokea jumamosi yanaonesha kuwa hali ya kisiasa inaendelea kuwa mbaya wakati kukisalia miezi kadhaa ili chaguzi za mwaka 2015 zifanyike.

Marekani, kwa upande wake, imelani vikali nguvu ziliyotumiwa na polisi dhidi ya upinzani, pamoja na kitendo cha kuwateka askari polisi.

Upinzani unapinga utawala wa Pierre Nkurunziza kwa kutaka kubadili kwa makusudi katiba ya nchi ambayo ilipatikana kupitia mazungumzo ya amani yaliyopelekea kusitishwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe (1993-2006), viliyosababisha zaidi ya watu 300,000 kupoteza maisha.

Hayo yakijiri, chama cha UPRONA, ambacho kina wafuasi wengi kutoka jamii ya watutsi ni chama kimoja pekee kiliyoshiriki chaguzi za mwaka 2010 pamoja na chama cha CNDD-FDD, kilijiondoa serikalini hivi karibuni , baada ya viongozi kujaribu kukisambaratisha kutokana na msimamo wake wa kupinga marekebisho ya katiba.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.