Pata taarifa kuu
MYANMAR-Msamaha

Mashirika ya haki za binadamu yapongeza serikali ya Myanmar kutangaza kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa

Serikali ya Myanmar imetangaza kuwaacha huru wafungwa wote wa kisiasa ikiwa ni hatuwa muhimu katika kuendelea kujikwamuwa kuondoka katika vikwazo dhidhi ya jumuiya ya kimataifa. Serikali ya Rangoon imesema hakuna tena mfungwa wa kisiasa katika jela. Hata hivyo bado kuna hali ya wasiwasi juu ya hatma ya wafungwa hao na wengine takriban mia mbili wanaosubiri kusikilizwa kwa kesi zao.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa rais wa taifa hilo Ye Htut amesema, rais Thein Sein ametekeleza ahadi yake kwa wananchi ya kwamba hakutokuwa na mfungwa wa kisiasa baada ya mwaka 2013. hata hivyo haikutajwa idadi ya wafungwa waliaoachwa huru kufuatia hatuwa hiyo ya msamaha wa rais na lini wataondoka jela.

Duru sahihi zimethibitisha kuwa takriban wafungwa tisa wa kisiasa wameachiwa huru hapo jana, miongoni mwao ni Yan Naing Tun aliye katika hukumu ya kifungo cha miezi minane kwa kutuhumiwa kushiriki katika maandamano ya amani jimboni Kachin lenye kukumbwa mara kadhaa na mashambulizi baina ya majeshi ya serikali na kundi la waasi kaskazini mwa Myanmar.

Yan Naing Tun aliwaambia waandishi wa habari kwamba anamuheshimu rais wa nchi hiyo baada ya kutekeleza ahadi yake.

Viongozi wa mashirika yanayo tetea haki za kibinadamu hususan Human Right Watch kupitia mmoja wa vingozi wake David Mathieson, amesema wameridhishwa na hatuwa hiyo na kusema kwamba ni ya muhimu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.