Pata taarifa kuu
THAILAND

Baada ya wabunge wote wa upinzani kujiuzulu, Waziri Mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra aahidi kuvunja bunge na kuitisha uchaguzi

Waziri mkuu wa Thailand Yingluck Shinawatra amesema atavunja bunge na kuitisha uchaguzi mara moja baada ya maandamano na vurugu kuendelea kutikisa mji mkuu wa nchi hiyo Bangkok. Hatua hiyo inafuatia kujiuzulu kwa wabunge wote wa upinzani siku ya Jumapili, na mipango ya kufanyika maandamano makubwa dhidi ya serikali siku ya jumatatu.

REUTERS/Dylan Martinez
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha televisheni leo jumatatu, Yingluck amesema uchaguzi pekee ndio utakuwa njia sahihi kwa watu wa Thailand kuamua kile wanachokitaka.

Baada ya ghasia na maandamano kwa takribani mwezi mmoja Yingluck amesema uchaguzi huo ukafanyika mwishoni mwa mwezi January au February mwaka ujao.

Waziri Yingluck amesema watu wengi wa makundi mbalimbali wanapinga serikali na njia bora ni kuwapa nafasi watu wa Thailand kuamua kupitia uchaguzi.

Hata hivyo waandamanaji wameapa kuendelea na maandamano kwa madai kwamba serikali ya Yingluck inaongozwa na kaka yake Thaksin Shinawatra, ambaye anaishi uhamishoni baada ya aliondolewa mamlakani.

Kiongozi wa maandamano hayo, Suthep Thaugsuban amesema hatasitisha maandamano hayo mpaka azma yao itakapokamilika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.