Pata taarifa kuu
THAILAND-Maandamano

Kiongozi wa waandamanaji Suthep Thaugsuban awataka waandamanaji kuchukua udhibiti wa makao makuu ya Polisi Bankok

Kiongozi wa waandamanaji nchini Thailand Suthep Thaugsuban amesema kuwa maandamano hayo yataendelea hadi pale Waziri Mkuu Yinluck Shinawatra atakapojiuzulu.

Kiongozi wa waandamanaji nchini Thailand Suthep Thaugsuban
Kiongozi wa waandamanaji nchini Thailand Suthep Thaugsuban REUTERS/Damir Sagolj
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo ametoa wito kwa waandamanaji kuchukua udhibiti wa makao makuu ya Polisi jijini Bangkok muda mfupi baada ya waandamanaji hao kukabiliana na polisi wakati wakijaribu kuvamia ofisi za Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu Shinawatra amekataa shinikizo za waandamanaji hao la kujiuzulu na badala yake kuja katika meza ya mazungumzo.

Shinawatra anasema kuwa wito wa waandamanaji kutaka baraza la mpito kuteuliwa ili kuongoza serikali haukubali na ni kinyume cha Katiba.

Mahakama Kuu nchini humo imetoa hati mbili ya kukamatwa kwa kiongozi wa maandamano hayo bila mafanikio licha ya kuonekana jana jijini Bankong akitoa hotuba kwa waandamanaji.

Waandamanaji hao wanasema kuwa wamechoka na uongozi wa Waziri Mkuu Shinawatra wanaosema kuwa unaongozwa na kakake Thaksin Shinawatra aliyeondolewa madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.