Pata taarifa kuu
THAILAND-Maandamano

Maandamano Thailand;Waziri mkuu Shinawatra apuuza shinikizo la kujiuzulu

Waziri mkuu wa Thailand Yingluck Shinawatra ametupilia mbali shinikizo la waandamanji linalomtaka kujiuzulu wakati huu kukishuhudiwa ghasia zikiibuka upya mjini Bangkok.

Waziri Mkuu wa Thailand Yingluck Shinawatra
Waziri Mkuu wa Thailand Yingluck Shinawatra rfi
Matangazo ya kibiashara

Waziri Yingluck amesema madai ya waandamanji hayawezekani kwa mujibu kwa katiba ingawa yupo tayari kwa mazungumzo.

Ghasi azaidi zimeibuka mapema jumatatu katika harakati za waadamanaji kurushia mawe ofisi ya waziri mkuu ambayo ni ofisi ya serikali.

Takribani watu wanne wameuawa katika ghasia hizo za kisiasa mbaya kutokea tangu mwaka 2010 maandamano yalipoishia kuwa vurugu.

Katika taarifa yake Yingluck amesema yupo radhi kufanya lolote kuwafurahisha raia wake vinginevyo hawezi kufanya chochote kinyume na katiba.

Maandamano hayo yameendelea kushinikiza kujiuzulu kwa waziri mkuu Yingluck huku kiongozi wa maandamano hayo na mwanasiasa wa upinzani wa zamani Suthep Thaugsuban akisema Yingluck ni lazima ajiuzulu ndani ya siku mbili.

Waandamanaji wanataka kuuweka mamlakani utawala ambao haujachaguliwa kisheria maarufu kama ''People's Council",kwa madai kwamba serikali ya waziri Yingluck inaongozwa na kaka yake aliyeondolwa madarakani Thaksin Shinawatra.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.