Pata taarifa kuu
THAILAND

Polisi wapambana na waandamanaji waliovamia majengo ya serikali wakitaka kumuondoa Waziri Mkuu wa Thailand

Polisi nchini Thailand wametumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya waandamanaji waliotaka kuvamia majengo ya serikali wakitaka kumuondoa Waziri Mkuu Yingluck Shinawatra. Hofu ya usalama imezidi kuwa kuwa kubwa nchini humo baada ya waandamanji wawili kuuawa na wengine takribani 45 kujeruhiwa katika ghasia za siku ya jumamosi.

REUTERS/Dylan Martinez
Matangazo ya kibiashara

Vifo hivyo ni vya kwanza kuripotiwa toka kuanza kwa maandamano ya amani takribani mwezi mmoja, kila upande umekuwa ukilaumu mwingine kuwavamia wafuasi wake.

Serikali ya Thailand imepeleka wanajeshi zaidi ya 2700 kuimarisha usalama katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangkok.

Waandaaji wa maandamano hayo wametoa wito kwa wafuasi wao kurejea katika maandamano makubwa zaidi hii leo ili kuendeleza harakati za kumng'oa madarakani Waziri Mkuu Yingluck Shinawatra ambaye mwenyewe hajaonesha utayari wa kuachia madaraka.

Awali viongozi wa waliwataka waandamanaji kurejea nyumbani kwa muda ili kuepusha madhara zaidi wakati wakiandaa mikakati kabambe ya kumuondoa madarakani Waziri Mkuu Yingluck.

Ghasia dhidi ya utawala wa Yingluck zimechochewa na hatua ya kiongozi huyo kuwasilisha bungeni muswada unaolenga kumsamehe kaka yake na Waziri Mkuu wa Thaksin Shinawatra anayeishi uhamishoni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.