Pata taarifa kuu
Thailand

Waandamanaji nchini Thailand kuandama leo kuelekea makao makuu ya chama tawala

Waandamanaji nchini Thailand leo Ijumaa wamepanga kuandamana kuelekea makao makuu ya chama tawala cha waziri mkuu Yingluck Shinawatra, licha ya kiongozi huyo kuahidi kushirikiana na wapinzani na kuomba wajadiliane ili kumaliza mgogoro wa kisiasa unaotokota hivi sasa.

Waandamanaji nchini Thailand
Waandamanaji nchini Thailand RFI
Matangazo ya kibiashara

Wito wa waziri mkuu Yingluck Shinawatra ni kama umechochea zaidi waandamanaji kuzidisha ghasia na hata kuharibu miundo mbinu ya umeme katika makao makuu ya polisi nchini humo.

Waziri mkuu Shinawatra bado ana kibarua kigumu katika utatuzi wa ghasia hizo, licha ya kura ya kutokuwa na imani naye kushindwa kupata uungwaji mkono bungeni baada ya wabunge wengi wa chama tawala kumuokoa hiyo jana.

Tuhuma dhidi ya kuwasilisha bungeni muswada unaolenga kumsamehe kaka yake na waziri mkuu wa zamani Thaksin Shinawatra umezidi kufifisha imani ya kiongozi huyo kwa wananchi.

Kumekuwa na hofu huenda taifa hilo likatumbukia katika machafuko zaidi kama ilivyoshuhudiwa mwaka 2006 wakati wa harakati za kuung'oa utawala wa kaka yake Thaksin.

Wapinzani wa Yingluck wanataka taifa hilo lihakikishe Thaksin anayekabiliwa na tuhuma za makosa mbalimbali yakiwemo ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka wakati wa utawala wake harejei nchini humo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.