Pata taarifa kuu
AFGHANSTAN-MAREKANI-usalama

Marekani yaonya Afghanistan kuchelewesha kusaini mkataba mpya wa usalama

Marekani imeionya Afghanstan kuhusu kusaini mkataba mpya wa usalama haraka iwezekanavyo wakati huu ambapo wakuu wamekuwa wakigusia kuwa ucheleweshwaji wa suala hilo kutasababisha Marekani kuyaondoa majeshi yake baada ya 2014.

Raisi wa Afghanstan Hamid Karzaï akiwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry jijini Kabul.
Raisi wa Afghanstan Hamid Karzaï akiwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry jijini Kabul. REUTERS/Mohammad Ismail
Matangazo ya kibiashara

Takriban wajumbe elfu mbili na mia tano wamekutana katika bunge la Afghanistan kujadili juu ya mpango wa serikali ya Kaboul na Marekani kuhusu Usalama wa Afghanistan baada ya kufikia makubaliano.

Wajumbe hao wanachambua kwa kina kuhusu makubaliano yaliofikiwa na Marekani kuhusu mpango wa Usalama wa nchi hiyo baada ya wanajeshi wa kigeni waliopo nchini humo kuondoka mwishoni mwa mwaka 2014.

hata hivyo Marekani imefahamisha kwamba haijachukuwa uamuzi wowote juu ya baadhi ya wanajeshi wake kadhaa kubaki nchini humo baada ya muda wake kumalizika mwaka 2014, licha ya kufikia makubaliano na serikali ya Kaboul kuhusu Usalama wa taifa hilo.

Serikali ya Washingon imeitaka Kabul kuharakisha haraka iwezekanavyo juhudi za kutafuta muafaka na kupatikana kwa makubaliano kabla ya mwaka huu kumalizika na kukubaliana juu ya idadi ya wanajeshi wa Marekani wataobaki nchini Afghanistan mwaka 2015.

Hapo jana rais wa Afghanistan Hamid Karzai alithibitisha kuwa wanajeshi elfu kumi na tano wa kigeni huenda wakasalia nchini humo baada ya muda wa kuwepo vikosi vya nchi za Jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi NATO kumaliza muda wake mwishoni mwa mwaka 2014.

Upande wake Marekani kupitia msemaji wake wa mambo ya nje Jennifer Psaki imeitaka Afghanistani kuharakisha mchakato wa kupatikana kwa makubaliano kabla ya mwishoni mwaka 2013.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.