Pata taarifa kuu
AFGHANSTAN-usalama

Afghanstan kuamua mpango wa usalama kati yake na Marekani

Takribani wanajeshi 15,000 wa kigeni watabaki nchini Afghanistan baada ya mwaka 2014 ikiwa Marekani itakubaliana na mpango wa usalama kwa mujibu wa raisi wa Afghanstan Hamid Karzai.

Raisi wa Afghanstan Hamid Karzaï akiwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry jijini Kabul.
Raisi wa Afghanstan Hamid Karzaï akiwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry jijini Kabul. REUTERS/Mohammad Ismail
Matangazo ya kibiashara

Raisi huyo ameyasema hayo katika mkutano na zaidi ya wakuu elfu mbili ambao walikusanyika kujadiliana kuhusu mpango huo wa usalama.

Moja kati ya hoja za msingi ni mazingoira ambayo majeshi ya Marekani yatakuwa yakiingia katika makazi ya Afghan.

Hoja nyingine ni ikiwa majeshi ya Marekani yatawajibika kwa Mahakama za Marekani au za Afghanstan.

Hata hivyo rasimu ya makubaliano uliotolewa Kabul kabla ya kuanza kwa mkutano huo uliashiria kwamba raisi Karzai aliridhia kwamba Majeshi ya Marekani yatawajibika katika mahakama za nchini humo.

Kulingana na hati ya Kabul Afghanistan imeamuru Marekani kufungua kesi au kuchukua hatua za yoyote ya kinidhamu ifaayo katika nchi ya Afghanistan.

Kulingana na rasimu ya makubaliano mpango huo utatumika hadi kufikia mwisho mwa 2024 na na kuendelea.

Kwa Sasa majeshi ya kimataifa ya Nato yanataraji kuondoka Afghanistan kuanzia 2014.

Katibu wa Marekani John Kerry alisema Jumatano timu yake imekubaliana kwa maandishi na Viongozi wa Afghanistan, ingawa haikuwa wazi kama rasimu ya Kabul ndiyo ilitiliwa maanani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.