Pata taarifa kuu
PAKISTAN-AFGANISTAN

Rais wa Afghanistan Hamid Karzai aomba msaada wa Pakistan kuzungumza na Taliban

Rais wa Afghanistan Hamid Karzai anaitaka serikali ya Pakistan kuwa katika mstari wa mbele kufanikisha juhudi za kuleta amani kati ya Afghanistan na kundi la Taliban.

Matangazo ya kibiashara

Karzai ambaye amezuru Pakistan amesema kuwa, Islamabad ina nafasi kubwa ya kuhakikisha kuwa kundi la Taliban linakuja katika meza ya mazungumzo kutokana na uhusiano wake mzuri na Taliban na amani ya kudumu inapatikana.

Waziri Mkuu mpya wa Pakistan Nawaz Sharif kwa upande wake amesema kuwa yeye atafanya kila kilicho ndani ya uwezo wake kuhakikisha kuwa amani inapatikana katika eneo hilo pamoja na nchi jirani ya Afganistan.

Imekuwa ziara ya kwanza kwa Karzai kuzuru Pakistan tangu kuchaguliwa kwa Waziri Mkuu Sharif suala ambalo wachambuzi wa siasa na usalama wanasema ni mwanzo wa kuimarisha uhusiano wa  mataifa hayo mawili ambayo yameonekana kutoamiana kwa kipindi kirefu.

Karzai ameeleza kuwa ana matumaini kuwa uongozi wa Pakistan kwa kiasi kikubwa utasaidia kuinua hali ya usalama kati ya mataifa hayo mawili.

Afghanistan inaamini kuwa serikali ya Pakistan imeendelea kutoa hifadhi kwa wafuasi wa kundi la Taliban kwa kipindi kirefu.

Aidha, Karzai ameitaka Pakistan kuwa mpatanishi wa mzozo kati yake na wanamgambo wa Taliban wito ambayo Pakistan imesema itatekeleza.

Kundi la Taliban limesema haliwezi kuzungumza na rais Karzai kwa madai kuwa yeye ni kibaraka cha Maraekani.

Juhudi za Karzai kutaka mazungumzo na Taliban zinafanyika miezi miwili baada ya mazungumzo yaliyokuwa yamepangwa kufanyika nchini Qatari kati ya serikali ya Afghanistan na Taliban kugonga mwamba mwezi Juni.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.